Tafakuri tunduizi ya Dk, Hamisi Kigwangala Mbunge wa Nzega , Aliyotoa facebook 19 feb 2012 .
Alianza kwakusema hivi...!!!
Leo nimeamka nikimfikiria kijana wa kitanzania. Haswa baada ya kupokea maombi ya vijana 6 kwa sms wakitaka niwasaidie kupata mahala pa kujishikiza, kwa 'marafiki zangu'. Mtihani huu mgumu sana. Nitautatuaje? Marafiki zangu kila siku wanatoa nafasi za ajira kwenye mashirika yao? Nikasema, labda tuanzishe mjadala mahsusi wa kitaifa, utakaolitazama suala la ajira kwa vijana wa kitanzania kwa mapana na marefu, na kulifanyia utekelezaji. Vijana wa zama hizi hawataki maneno, wanataka vitendo. Maneno na mipango mizuri iliyoandikwa haitowasaidia sana, wanahitaji fursa za ajira, za kujiajiri, za kuendesha maisha yao. Tena vijana wa siku hizi hawako tayari kutumiwa na wanasiasa kwa faida za kisiasa.
Hii ni Tafakuri Tunduizi yangu juu ya ufumbuzi wa tatizo la ajira kwa vijana na pia kukuza uchumi wa nchi yetu. haimaanishi hii ndiyo kila kitu na kwamba lazima vijana wote watataka kuwekeza kwenye industry nilizozitaja hapa, hii ni dira tu;
Tuanzishe mfuko maalum wa kutoa mikopo ya uwekezaji kwa vijana wa kitanzania. Mfuko huu utawalenga vijana watakaowekeza kwenye sekta ambazo tutazichagua, sana sana tutoe kipaumbele kwenye sekta za kilimo na viwanda vyenye backward au forward linkage na kilimo, moja kwa moja. Vijana hawa waingizwe kwenye challenge ya kupata mikopo, ambayo itatakiwa iwe na masharti nafuu, iwe na riba ndogo (asimilia 8 kushuka chini), iwe na payback period ndefu, ya miaka 15-20, isiwe na masharti ya dhamana/security za mali (maana vijana hawana assets zozote!) bali iwe na dhamana nafuu kama cheti cha elimu ama ardhi (shamba lililorasimishwa). Mpango huu uendane na kutengeneza utaratibu mzuri na rahisi wa kusajili mashamba. Yatengwe maeneo maalum ya kuwekeza. Vijana wawe guided kuwekeza kwenye sekta zilizochaguliwa na wawezeshwe kupata mitaji hiyo. Kama tutakuwa na vijana wataowezeshwa kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda kama vya kuchambua pamba, kukoboa na kusaga unga/chakula cha mifugo, kukamua na kusafisha mafuta ya kula, pia kutengeneza sabuni, kusindika juice, viwanda vya nyuzi (spinning mills), tutaweza kuwataka wawekezaji hawa vijana kuhamasisha kilimo cha kisasa na kusupport wakulima kwenye maeneo yao (linaweza kuwa sharti mojawapo la kupata mikopo hii maalum kwa ajili ya vijana) kwa kuwa-supply farm inputs, farm machinery, improved seed varieties etc - hii itasaidia kuongeza tija na ufanisi kwa wakulima.
Pamoja na kuongeza tija na ufanisi (productivity and efficiency), tutakuwa tumeongeza volume of farm and industrial produces (uzalishaji), uhakika wa soko utakuwepo (market stability and sustainability) na hatutouza mazao fresh kutoka shambani bali tutauza finished goods au semi-processed goods ambazo zimefanyiwa value addition kwenye viwanda vyetu; finally tutakuwa tumetatua tatizo si tu la ajira bali hata la kiuchumi kwa kuongeza uzalishaji, kuongeza thamani ya mazao yetu, kuhakikisha masoko ya uhakika kwa wakulima wetu na mwishowe kupunguza inflation ya vitu na zaidi zaidi kuongeza exports na kupunguza imports kitu ambacho kitasaidia ku-stabilise our BOP (balance of payments) account. Hapa pia tutakuwa tumetatua tatizo la kuanguka thamani kwa shilingi yetu. Ukiongelea kuimarisha uchumi wa nchi basi ni lazima uongelee kuongeza tija na ufanisi ambao utaongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa zenu, na wala siyo austerity measures za muda mfupi zinazopelekea kuimarisha fedha na viwango vyetu vya exchange rate against other foreign currencies. Ukiuangalia mpango huu utagundua kwamba kutakuwa na vijana wasomi (watakaoandaliwa kuwekeza kwenye viwanda) na wale ambao hawajasoma (watakaowekeza kwenye kilimo), haya makundi yatabebana - kwenye model hii, na hivyo kila kundi litatoa ajira kwa watu wengi zaidi.
Kwa nini basi mimi hapa napendekeza mikakati hii iwalenge vijana? Vijana, tukiondoa factors nyingine, kibaiolojia tunawategemea bado watakuwepo kuwepo hapa duniani kwa muda mrefu kidogo kuliko makundi mengine, na hivyo kama tutaendelea kuwa na uchumi unaokuwa kwa kasi hii ndogo na usiwaowashirikisha vijana kwa maksudi, maana yake wataishi maisha yao yote ya ujana, ujuzi, nguvu na ndoto kwa shida sana bila kutumika ipasavyo. Pia, ili kuwa na uchumi imara, ni lazima tujipange kwa kuangalia mbali kidogo, siyo kwamba tunafanya nini leo ili tufanikiwe leo! Tukiwatumia vijana kwa kuona mbele, wakiwekeza leo na wafanikiwa kuendesha biashara zao kwa faida maana yake ni kwamba baada ya miaka 20, Tanzania itakuwa na matajiri wengi zaidi, na itatoka kwenye kundi la nchi za daraja la tatu! Pia, ni rahisi sana kwa kijana kuchukua risk na kufanya kazi kwa bidii kufikia ndoto zake bila wasiwasi, na zaidi kundi hili likopewa kipaumbele linaweza kuibadili kabisa culture ya watanzania kutoka kwenye 'business as usual' na 'laissez-faire' na kuwa nchi ya watu wenye kufanya kazi kwa ubunifu wa hali ya juu na passion ya ukweli. Mimi naliona hili ndiyo kundi pekee litakaloweza kuijenga Tanzania mpya, Tanzania ya miaka 20 ijayo... haimaanishi wazee 'wa busara' wasiwepo kabisa, hapana lakini kwenye mpango huu wa kujenga upya viwanda vyetu na kutoa ajira kwa vijana, wasihusike.
Ni lazima tuwe na ndoto. Ni pia ni lazima tujipange kuzifikia ndoto zetu. Hakuna ujanja mwingine. Hatuwezi kufanikiwa kwa kutumia mikakati ile ile iliyotufikisha hapa. Huwezi kupanda mchicha ukajiandaa kuvuna bangi! Tunahitaji kubadilika, tunahitaji new approaches, new ideas... tukiwa na new approaches sasa hapo tunaweza kuona new results!.
HIZO NDO BUSARA ZA DK, HAMISI KIGWANGALA, natamani tungepata wabunge kama hawa 25 ivi wa CCM pale bungeni ingekuwa changamoto nzuri sana na mafanikio tungeyaona sana tena sana,
Hongera wapiga kura wa Nzega maana naamini walichagua Jembe la Kilimo bora sasa mlitunze tu ili litoe mavuno mema, Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Africa na Dunias nzima.
asante kutembelea peterdafi.blogspot.com, KARIBU TENA NA TENA....!!!!
No comments:
Post a Comment