Pages

Monday, May 28, 2012

CAMP MULLA KUWANIA TUZO ZA BET


Kituo cha televisheni cha Marekani cha BET (Black Entertainment Television) kimetangaza majina ya watakaowania tuzo za mwaka 2012.

Waliotajwa katika kipengele cha Best International Act Africa, ni pamoja na kundi la Camp Mulla la Kenya linaloundwa na vijana watatu.

Kutajwa kuwania tuzo za BET kwa kundi hilo ambalo Jumapili iliyopita liliacha gumzo nchini Afrika Kusini kutokana na show yake ya kufa mtu katika siku ya eviction ya Big Brother Africa, kumeliwekea historia nyingine ukizingatia kuwa lilianza kujulikana mwaka jana pekee.

Kundi la Camp Mulla linalofanya hip-hop linaundwa na Taio Tripper, Young Kass, Super-Producer K’Cous, Miss Karun, na Tuchi. Nyimbo zilizowatambulisha zaidi Camp Mulla ni pamoja na , Party Don’t Stop, Addicted, Holding it Down na Fresh All Day ambazo huoneshwa kwenye vituo vikubwa vya televisheni kama BET International, MTV Base, Trace TV na Channel O.

Camp Mulla wameweka historia ya wanamuziki wa Afrika Mashariki kuwahi kutajwa kuwania tuzo za BET jambo litakalolifanya kundi hili kuwa kundi maarufu zaidi barani Afrika kutokana na kuwa na vijana wadogo wenye vipaji visivyo na kifani.

Wasanii wengine wa Afrika waliotajwa kwenye kipengele hicho cha Best International Act ni pamoja na Panshak Zamani, aka Ice Prince na Ayodeji Ibrahim Balogun; a.k.a Wizkid wa Nigeria, Lira wa Afrika Kusini,Mokobe wa Mali, Sarkodie wa Ghana

No comments:

Post a Comment