Frances ambaye aliwahi kukutana na Rais Kikwete wakati wa ufunguzi wa jengo la Tanzania House katika jiji la Washington DC amesema kuwa ni nadra sana kuona kiongozi wa nchi akikutana na viongozi wa chama cha mchezo wowote kuzungumzia maendeleo yake. Hii ni miujiza hata katika nchi kama Marekani.
Marie Frances amemuelezea Rais Kikwete kama mtu wa haiba ya kipekee mwenye akili na maono ya kuiendeleza Tanzania kufikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya Millenia. “Nilimpenda sana nilipokutana naye jijini Washington. Ni kiongozi mwenye haiba ya kipekee” alisema Frances ambaye aliombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri kuja kuanzisha mbio za marathon nchini Tanzania mwaka 1990.
Marie Frances ambaye alikuwa mkuzaji (producer) wa Miss Universe pamoja na vipindi vya television huko Hollywwod nchini Marekani alihamia nchini Misri mwaka 1984 kuafanya kazi ya ABC kama mwandishi wa bahari. Akiwa nchini Mirsi, Marie Frances alianzisha mbio za Pyramid Marathon pamoja na Miss Universe ambazo ziitangaza sana nchi ya Misri. Ni wakati wa matamasha haya balozi wa Tanzania nchini Misri wakati huo alipomwomba aje Tanzania kuanzisha mbio za marathon ili kuitangaza Tanzania.
Frances alikuja Tanzania mwaka 1990 na kutaka kuanzisha mbio za Mt. Meru Marathon lakini alipofika tu mjini Moshi alivutiwa sana na mlima Kilimanjaro na hivyo kuiamua kuanzisha mbio za “Mt. Kilimanjaro Marathon” mwaka 1991. Mbio hizi hukimbiwa kila jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita na zitatimiza miaka 22 tarehe 24 Juni mwaka huu.
Mt. Kilimanjaro Marathon zimeshapewa tuzo mbalimbali kama mbio za kimataifa. Gazeti la Wonders of the World lenye wasomaji zadi ya million 5 limezipa nafasi ya 2 kama mbio nzuri za kushiriki. Wakati jarida la kimataifa la Forbes limezipa nafasi ya kwanza kama mbio nzuri za kukimbia! Marie Frances pia ameanza kuwapeleka wanariadha wa Tanzania kukimbia nchini Marekani kwa kuwasaidia fedha za Visa za Marekani pamoja na tiketi za ndege kama inavyoonyesha picha ambapo mkimbiaji Nelson Brighton anapewa pesa na Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Benadetta Kinabo kwenda nchi Marekani mwezi ujao kwa ufadhili wake.Kwa sasa mbio hizi hufadhiliwa na shirika la ndege la Ethiopia.
Ni katika juhudi zake za kuutangaza mlima Kilimanjatro ndipo Manispoaa ya Moshi ikaipa jina la Marie Frances Boulevard barabara ya zamani ya Bustani Ale.
Mt. Kilimajaro Marathon itaanzia Moshi Klabu tarehe 24 Juni saa kumi na mbili asubuhi ambapo mbio za kilometa 42, 21, 10 na 5 zitashindaniwa na watalii toka Marekani pamoja na wakimnbiaji toka Moshi na Arusha.
Wakimbiaji wanajiandikisha kwa wingi Bristol Cottages hotel iliyopo mkabala na benki ya Standard Chattered karibu na Kilimanjaro Hospital katika Manispaa ya Moshi.
No comments:
Post a Comment