KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles
Kenyela, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la kuwania ubingwa
wa Afrika Mashariki na Kati baina ya Thomas Mashali wa Tanzania na Medi
Sebyala wa Uganda litakalopiganwa Oktoba 14,Siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa la Tanzania kwenye ukumbi wa Friends
Corner Manzese jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam , Mratibu
wa pambano hilo linalosimamiwa na Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa
Tanzania (TPBO), Regina Gwae, alisema mbali Kamanda Kenyela, kutakuwa na
wageni wengine maalum akiwemo Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan.
Alisema wanashukuru kwa ushirikiano wa viongozi hao katika maandalizi
na hatimaye wamethibitisha ushiriki wao katika pambano hilo ambalo
linavuta hisia za watu wengi na wapenzi wa ngumi jijini Dar es Salaam.
Alitaja mapambano manne ya utangulizi ya siku hiyo ambapo Abdul Awilo
atazichapa na Shedrack Juma, Selemani Shaaban atavaana na Hamisi Mohamed
huku Jonas Segu akinyukana na Ibrahim Class wakati Charles Mashali
atatwangana na Teacher Aaron.
“Tumeamua kuchukua mabondia kutoka katika klabu zenye mashabiki wengi,
tumechukua kwa Mzazi tumechukua klabu ya manzese anakotoka Mashali na
Super D Boxing Club,’ alisema Regina.
Regina alisema, bondia Medi Sebyala na Kocha wake wanatarajiwa
kuwasili nchini Oktoba 11 na tayari maandalizi ya safari yao
yamekamilika, ikiwemo kuwatumia tiketi na wameshazipokea.
Mratibu huyo, aliishukuru kampuni ya Promasidor wasambazaji wa Sossi
Poa, Gazeti la Jambo leo, City Sports Lounge na Times Fm kwa kuwa bega
kwa bega kuhakikisha pambano hilo linafanikiwa na kuwa, milango bado iko
wazi kwa wadau kujitokeza kufanikisha mchezo huo ambao ni chanzo cha
ajira kwa vijana.
Super D, alisema katika mpambano huo
atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa
SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na
mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza
watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota
hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali
wengine DVD hizo zina michezo ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha
kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa
kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine
tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi
tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema.
Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya
mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia hii watu wengi
wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi
katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo. Aliongeza
kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza
kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa timu
ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli,
Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana mbalimbali
|
|
No comments:
Post a Comment