Majeshi ya Serikali
ya Somalia na Umoja wa Afrika AMISOM yameingia katikati ya mji wa
Kismayo siku chache baada ya wapiganajiwa wa Al Shabaab kuondoka katika
mji huo.
Msemaji wa jeshi la Somalia, ameelezea kuwa
mamia ya wanajeshi walihusika katika operesheni hiyo huku majeshi ya
AMISOM yakijiandaa kwa mapambano ya kuutwaa mji huo kutoka mikononi mwa
Al Shabaab.Kismayo ndiyo ilikuwa ngome ya mwisho ya Al Shabaab.
Hii ni mara ya kwanza kwa majeshi hayo kuingia katikati ya mji huo tangu operesheni ya kuwasaka Al Shabaab ilipoanza.
Wakaazi wanasema baada ya kuondoka kwa wapiganaji wa Al Shabaab hali ya usalama katika mji huo imekuwa sio ya kuridhisha ambapo kumekuwa na taarifa za baadhi ya viongozi maarufu wa koo kuawawa.
No comments:
Post a Comment