Mohamed Bin Hammam ametangaza
ramsi kuwa amejiuzulu kutoka kwa nyadhifa zake katika kamati kuu ya
shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA na pia kama rais wa shirikisho
la mchezo wa soka barani Asia, AFC.
Hamman, ameliambia shirika la habari AFP kupitia
barua pepe, kuwa amejiuzulu kutoka nyadhifa hizo siku Kumi, baada ya
kamati kuu ya maadili ya FIFA kuanzisha upya uchunguzi kuhusiana na
madai ya ufisadi dhidi yake.FFIA imethibitisha kupokea barua kutoka kwa Hamman ya kujiuzulu, lakini imekariri kuwa kamati yake ya madili imesalia kuwa uhuru na ina uwezo kwa kuchukua maamuzi kuhusiana na masuala mbali mbali, licha ya wanaohusika kujiuzulu.
Katika misingi hiyo, FIFA imesema ripoti yake ilionyesha kuwa Mohammed Bin Hamman, alikiuka kifungu cha 19 cha sheria zake wakati alipokuwa rais wa AFC na mwanachama wa kamati kuu ya FIFA, kati ya mwaka wa 2008 hadi mwaka wa 2012, hatua iliyopelekea kamati hiyo kumpiga marufuku ya kushiriki katika shughuli yoyote inayohusiana na mchezo huo maishani.
Hammam mwenye umri wa miaka 63, anatuhumiwa kujaribu kununua kura ili kuchaguliwa kuwa rais wa FIFA mwaka wa 2011.
Hata hivyo marufuku hiyo ilibatilisha na mahakama ya upatanishi ya Michezo CAS mwezi Juni kutokana na kile kilichotaja kama ukosefu wa ushahidi kuhusu madai hayo ya ufisadi.
No comments:
Post a Comment