Droo ya michuano ya raundi ya pili ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya imetolewa.
Manchester United imeratibiwa kuchuana na mabingwa wa Uhispania Real Madrid katika uwanja wa Old Trafford.Mechi hiyo itakuwa mechi ya kwanza kwa nyota wa Real Madrid na mchezaji wa zamani wa Manchester United Christiano Ronaldo katika uwanja huo tangu aliposajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 80 na klabu ya Real mwaka wa 2009.
Celtic itacheza na mabingwa wa Italia Juventus, Arsenal kupepetana na Bayern Munich ya Ujerumani.
Mabingwa mara nne wa kombe hilo Barcelona kucheza na mabingwa mara saba wa kombe hilo AC Milan nayo Valencia kutoa udhia dhidi ya Paris St Germain.
Borussia Dortmund imepangiwa kucheza na Shakhtar Donetsk, Porto kutoana jasho na Malaga, ili hali Galatasaray kucheza na Schalke 04.
Je United italipiza kisasi ya mwaka wa 2003?
Timu hizo mbili zilizkutana mara ya mwisho mwakwa wa 2002-2003 wakati wa robo fainali ya mashindano hayo ambapo Real ilishinda kwa jumla ya magoli 6-5.
Real ilishinda raundi ya kwanza kwa mabao 3-1 kalini katika mechi ya rauni ya pili uinted ilishind akatika uwanja wa Old Trafford kwa magoli 4-3.
Mechi za awamu ya kwanza zitachezwa kati ya tarehe 12 au 13 au tarehe 19 au 20 mwezi Februari na mechi za marudiano imepangiwa kuchezwa kati ya tarehe 5 -6 au 12-13 mwezi Machi mwaka ujao.
Droo Kamili
Galatasaray vs FC SchalkeCeltic vs Juventus
Arsenal vs Bayern Munich
Shakhtar Donetsk vs Borussia Dortmund
AC Milan vs Barcelona
Real Madrid vs Manchester United
Valencia vs Paris St Germain
FC Porto vs Malaga
No comments:
Post a Comment