Amin Salmin
*Adai si ndugu yao na hapaswi kutumia jina la Baba yake
MTOTO
wa pili wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Zanzibar, Dk. Salmin Amour, Amin
Salmin, ameibuka na kukanusha vikali kuwa 'Ndugu Jambazi' Kassim
Ramadhan Juma (27) aliyeripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari
kukamatwa kwa ujambazi kuwa si ndugu yao katika familia.
Akizungumza
na Mtandao huu wa www.peterdafi.blogspot.com, Amin, alisema kuwa
amesikitishwa sana na kijana huyo aliyeripotiwa katika vyombo vya habari
kwa tukio la ujambazi kwa kutumia vibaya jina la Baba yake wakati si
mtoto wa baba yake na wala hakuzaliwa na Baba yake na pia na ndiyo maana
anaita Ramadhan Juma.
Aidha
Amin alisema kuwa wakati mama yake na mtoto huyo anayejulikana kwa jina
la Salma Kasu, alipokuwa akiolewa na Baba yake mwaka 1990, tayari mtoto
huyo Kassim Ramadhan Juma, alikuwepo na alikuwa ana umri wa miaka, 22
ambapo hadi leo ana umri wa miaka 27.
''Wakati
Baba yangu akimuoa Mama yake na Ramadhan huyu kijana alikuwa na miaka
22, inamaana Baba yangu alimkuta mama yake akiwa tayari na mtoto mkubwa
tu, ambaye Mama yake alizaa na mume mwingine kabla ya kuolewa na baba
yangu,. sasa iweje leo ajiite mtoto wa Salmin tena katika mambo yake
mabaya yasiyofaa katika Jamii, si kutaka kumchafua tu Mzee wa watu na
kumpa mipresha ya bure, baba yangu''?. alihoji Amin.
Kwa
kubainisha usemi wake Amin, aliongeza kuwa anawatambua vilivyo nduguze
watatu, aliowataja kwa majina, kuwa ni Abal, Hamoud na Salama, ambao
wamezaliwa na mama wa Kassim Ramadhan Juma, na Baba yake mzazi Dkt.
Salmin Amour.
''Mimi
nawatambua ndugu zangu ambao Baba yangu amezaa na Mama wa Kassim
Ramadhan Juma, Salma Kasu, lakini huyu 'ndugu Jambazi' wala simtambui
katika familia yetu, na wala hajawahi kutokea kati yetu kutumia jina la
baba kwa 'Ujina na upuuzi' kama anavyofanya huyo ndugu Jambazi, Namuomba
sana huyo Kassim Ramadhan Juma, na wenzake wasiendelee kutumia jina la
Baba yangu kwa maovu yao kwani ni kutaka kumchafua tu baba yangu ambaye
haitaji kuwa na presha za namna hiyo kwa sasa''. alisema Amin
Habari Na Sufiani
No comments:
Post a Comment