Pages

Tuesday, January 22, 2013

Bafana Bafana tayari kuchuana na Angola

Mchezaji wa Angola Manucho
Baada ya kutoka sare ya kutofungana bao lolote katika mechi yao ya ufunguzi, ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika, wenyeji wa mashindano hayo Afrika Kusini, wanashuka uwanjani kwa mechi yao ya pili hiyo kesho na Angola.
Baada ya mechi yao ya kwanza kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya Afrika Kusini, Gordon Igesund, aliwashutumu wachezaji wake kwa kukosa umakini.
Igesund, ambaye ni kocha wa tatu kuliongoza Bafana Bafana, tangu michuano ya kombe la dunia mwaka wa 2010, alikiri kuwa wachezaji wake walionyesha mchezo mbaya katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Soccer City, mjini Johannesburg.
Igesund amesema baada ya mechi hiyo, wachezaji wake sasa ni sharti wacheze kadri ya uwezo wao na kushinda mechi zilizosalia ili kufufua matumaini yao ya kufuzu kwa raundi ijayo.
Kipa wa Afrika Kusini Itumeleng Khune
Angola vile vile ilitoka sare ya kutofungana bao lolote la Morocco katika mechi yao ya kwanza.
Mshambulizi wa Angola, ambaye alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza na timu hiyo ya taifa Guilherme Afonso, amesema sasa ana imani kuwa watashinda mechi hiyo.
Afonso, alionyesha mchezo mzuri katika mechi yao na Morocco na asema walijiufunza mengi kutoka kwa mechi hiyo.
Wakosoaji wengi wanahisi, Angola, ilipoteza nafasi nyingi za kufunga na wachezaji wake wakiwemo aliyekuwa mshambulizi wa Manchester United, Manucho, hawakucheza kadri ya uwezo wao.

No comments:

Post a Comment