Pages
▼
Thursday, February 28, 2013
CCM na CHADEMA kimewaka tena mkoani SHINYANGA wilaya ya KAHAMA
Chama cha demekrasia na maendeleo CHADEMA Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kinataraji kufanya maandamano ya amani marchi 02 mwaka huu, kuukumbusha uongozi wa mgodi wa Buzwagi kuwaunganishia umeme wananchi wa Kahama, kutoka katika mgodi huo.
Maandamano hayo pia yanalengo la kuukumbusha uongozi wa Mgodi kuishinikiza serikali kusiamamia utekelezaji wa ujenzi wa barabara za mji wa Kahama kwa kiwango cha lami.
Kufuatia chadema kutaka kufanya maandamano hayo chama cha mapinduzi kimesema chadema wanataka kufanya hivyo baada ya kupata taarifa kuwa tayari serikali ya ccm imeshakamilisha zoezi hilo na utekelezaji utaanza wakati wowote hivyo chadema wanataka kufanya maandamano ili umeme huo ukifikishwa kahama na barabara zikianza kujengwa waseme ni mafanikio ya maandamano yao.
lakini pia ccm wamesema chadema huenda wanataka kufanya maandamano ili kumuudhi muwekezaji huyo na kuchelewesha utekelezaji huo.
No comments:
Post a Comment