Pages

Wednesday, February 20, 2013

Kibarua cha mawakili kupata dhamana kwa Pistorius



Mawakili wa Pistorius wana kibarua kuishawishi mahakama kumpa dhamana mwanariadha huyo
Shahidi alisikia mayowe yakipigwa katika nyumba ya mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius kabla ya milio ya risasi kusikika tarehe 14 wakati wa mauaji ya mchumba wake.
Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Wendesha mashtaka wanaotaka kuhakikisha kuwa mahakama haimwachilii mwanariadha huyo kwa dhamana.
Pistorius anakabiliwa na kosa la kupanga mauaji ya mchumba wake, Reeva Steenkamp.
Jumanne Pistorius aliambia mahakama kuwa alimpiga risasi marehemu Reeva alipokuwa bafuni akidhania kuwa ni mwizi aliyekuwa amevamia nyumba yake.
Ni siku ya pili ya kesi itakayoamua ikiwa Pistorius atapewa dhamana au la.
Kesi ya mwanariadha huyo kwa kina haitarajiwi kufanyika hivi karibuni.
Bwana Pistorius aliwasili mahakamani hii leo akiwa ndani ya gari la polisi huku akijifunika kichwa chake kwa blanketi.
Kesi ilichelewa kidogo kufuatia msukumano wa waandishi na watu wengine wakijaribu kuingia mahakamani
Hata mwandishi mmoja alipoteza fahamu katika hali hiyo.
Tayari hakimu anayesikiliza kesi hiyo ameiweka kesi yenyewe katika daraja ya sita maana kuwa ni muaji yaliyokuwa yamepangwa.
Sasa kibarua kwa upande wa utetezi unastahili kushawishi mahakama kumpa dhamana Pistorius kwa misingi ya yaliyotokea hata akamuua mchumba wake.

No comments:

Post a Comment