Pages

Thursday, February 21, 2013

Wanafunzi wajiunga na mgomo Malawi



Viwanja vya ndege vimeathirika kutokana na mgomo wa wafanyakazi wa umma
Polisi nchini Malawi wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya wanafunzi wa shule waliokuwa wanashiriki maandamano huku mgomo wa wafanyakazi wa umma ukikithiri.
Mamia ya wanafunzi waliojawa ghadhabu kuwa mafunzo yao yameathirika walijiunga na maandamano hayo mjini Lilongwe.
Walimu ni miongoni mwa maelfu ya wafanyakazi wa umma ambao wamekuwa wakigoma tangu wiki jana wakitaka nyongeza ya asilimia sitini na saba ya mshahara kufuatia hatua ya serikali kushusha hadhi ya sarafu ya nchi mwaka jana.
Rais Joyce Banda, amesafiri kwenda Equatorial Guinea, kwa mkutano na rais wa nchi hiyo licha ya mgomo unaoendelea na ambao umesababisha kufungwa kwa viwanja rasmi ndege.

No comments:

Post a Comment