Pages

Thursday, March 21, 2013

Askofu mpya Anglikan duniani atawazwa



Askofu Mkuu Justin Welby
Askofu Mkuu Justin Welby ametawazwa rasmi kua Askofu Mkuu wa Cantebury .Kiongozi huyu wa umri wa miaka 57 ameapishwa rasmi ku mkuu wa Kanisa la England na kiongozi wa kiroho wa jamii ya waumini millioni 77 wa kianglikana duniani.
Katika ibada yake ya kwanza alisema kuna kila sababu ya kuwa na matumaini mema kuhusu mustakbala wa imani ya kikristo katika dunia yetu na hapa nchini.
"Kuna kila sababu ya kuwa na uhakika wa kuendelea kwa imani ya kikiristo hapa duniani na nchini mwetu."
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na mrithi wa kifalme ni miongoni mwa wageni elfu mbili walioalikwa katgika kanisa kuu la Canterbury.
Askofu Mkuu Welby aliwaambia : "changamoto zinazotukabili sasa za mazingira,uchumi maendeleo ya mwanaadamu na umasikini duniani ,zinaweza tu kukabiliwa na ushujaa kamambe uliokombolewa na ukristo.
Kwa mujibu wa utamaduni askofu alibisha mara tatu kabla ya kuingia ndani ya kanisa kuu. Alikiri kwamba watu huenda wakatofautiana kuhusu majukumu ya dola na mtu binafsi katika jamii yenye ufanisi.
Askofu Mkuu Welby ni Askofu wa 105th wa Canterbury.
Mwaandishi wa BBC wa maswala ya kidini , Robert Pigott, anasema Askofu mkuu mpya anarithi kanisa lilioshuhudia kupungukiwa na idadi ya waumini wanaohudhuria ibada katika miaka ya hivi karibuni na ambalo linajitahidi kuhubiri ujumbe wa ukristo katika jamii inayozidi kuonyesha kutotilia maanani maswala ya kidini .
Itachukuliwa kama ni jukumu lake kuliunganisha kanisa ambalo limekumbwa na migogoro kuhusu maaskofu wanawake na pengine hatari zaidi maswala ya ujinsia. .
Kwa mara ya kwanza katika historia ,mwanamke - Mchungaji Sheila Watson, ambae ni mkuu wa Mashemasi wa Canterbury - alishiriki katika moja ya hatua mbili za kutawazwa askofu mkuu

No comments:

Post a Comment