Meneja wa Biashara wa Nyumba ya vipaji Tanzania,THT, Kemilembe Mutahaba, akizungumza na mwanamziki kutoka Marekani,
Meneja wa Biashara wa Nyumba ya
vipaji Tanzania,THT, Kemilembe Mutahaba, akizungumza na mwanamziki
kutoka Marekani, Maya Azurenca ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku saba
katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya mwanamke duniani. Maya
alitembelea THT leo ambapo alishiriki mjadala kuhusu changamoto
zinazowakabili wasanii wanawake katika soko la muziki Tanzania
THT
yaandaa mjadala kuhusu changamoto zinazowakumba wasanii wa kike, pamoja na
mwanamziki wa kimarekani,Maya Azurenca.
Katika kuelekea maadhimisho
ya kilele cha siku ya kimataifa ya wanawake duniani, leo Nyumba ya vipaji
Tanzania, THT, imeandaa majadiliano kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo
wasanii wa kike hapa nchini, mjadala uliohusisha wasanii wa kike kutoka
THT,wasichana kutoka nyumba ya kulelea watoto yatima wa KIWOHEDE na mwanamuziki
kutoka Marekani, Maya Azurenca ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku saba.
Mjadala huo pia ulitoa
fursa kwa kinadada walio kwenye muziki, kama Mwasiti, Trio, Linah, Vumi na
Rachel kuelezea changamoto na uzoefu wao katika tasnia ya muziki.
Mjadala huo uliwapa nafasi
kina dada wanamuziki wa Tanzania kujifunza kutoka kwa Maya, ambaye ni
mwanamuziki wa muda mrefu kutoka Marekani.
Maya Azurenca akibadilishana mawazo na
wasanii kutoka THT
Maya ambaye pia ni balozi
wa utamaduni, ameimba nyimbo mbalimbali zinazohusu haki za binadamu na pia amefanya
matamasha nchi nyingi duniani kwa lengo la kuhamasisha kuhusu haki za binadamu.
Katika mjadala huo,
wasichana waliozungumza walisema kinadada katika tasnia ya muziki wanakumbwa na
changamoto nyingi na pia ni vigumu kwa waimbaji wa kike kupata fursa ya
kufanikiwa kulinganisha na wenzao wakiume.
Wakizungumza katika mjadala
huo, mwanamuziki wa kundi la kike la TRIO, Angela Karashani, alielezea
changamoto kubwa ambayo anakumbana nayo ni watu kudhani wao ni wahuni hasa kwa
kuwa wanajihusisha na muziki.
The Trio, alipowatembelea ofisini kwao leo asubuhi.
‘Ukiwa mwanamuziki wa kike
kwanza huwa ni shida sana kupata sapoti, lakini pia watu wengi wanachanganya
muziki na uhuni, ukiwa mwanamuziki wengi wanakufata wakidhani wewe ni mhuni
pia’ alisema Angela.
Mwanadada Maya aliwapa
chanagamoto kinadada hao wanamuziki kwa kuwaambia kuwa waweke juhudi katika
muziki na hakika watafika mbali.
‘Kitu kikubwa ambacho
nimejifunza kwenye maisha yangu ya muziki na ningependa kuwaambia hapa ni kuwa
kuwa mwanamuziki wa kike sio jambo rahisi, lakini kikubwa ni kuamini kile
unachofanya na kuweka juhudi katika hilo na kujiamini’ alisema Maya.
Mwanamuziki huyo pia ametoa
fursa ya kufanya nyimbo kadhaa na wanamuziki wa kitanzania wakati wa ziara yake
hii hapa nchini ili kuwapa fursa ya muziki wao kusikika kimataifa zaidi.
Wakati huo huo pia, uongozi
wa nyumba ya vipaji Tanzania, umetoa shukrani za pekee kwa ubalozi wa Marekani
Tanzania ambao ndio wamewezesha safari ya mwanamuziki huyo hapa nchini.
Akiwa THT pia alipata fursa ya kushiriki mjadala
kuhusu changamoto zinazowakabili wanamuziki wa kike hapa nchini.
No comments:
Post a Comment