Wanajeshi 13 wa Afrka
Kusini waliuawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati waasi
walipouteka mji mkuu, Bangui, Jumapili. Haya yalitangazwa na Rais Jacob
Zuma.
Bwana Zuma alisema Afrika Kusini "inajivunia" wanajeshi wake waliopambana na "waasi".Bwana Zuma alisema wanajeshi wengine 27 walijeruhiwa, na mmoja hajulikani alipo.
"Ni kipindi cha huzuni kwetu sisi… Twajivunia wanajeshi wetu 200 waliopambana na waasi," aliuambia mkutano wa waandishihabari katika mjii mkuu, Pretoria.
Msemaji wa waasi hao, Erick Massi, aliiambia BBC kwamba kiongozi wa Seleka, Michel Djotodia, ambaye ameshajitangaza kuwa rais, anapanga kufanya uchaguzi wa kidemokrasia, lakini hajasema utafanywa lini.
No comments:
Post a Comment