Pages
(Move to ...)
Home
▼
Thursday, April 4, 2013
BASHE CHUPUCHUPU KUTEKWA.....!.
WIMBI la viongozi wakuu wa
Kampuni ya New Habari (2006)
Ltd, kuendelea kuwindwa na
watu wasiofahamika,l imeendelea
kushika kasi baada
ya usiku wa kumkia jana,Ofisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni
hiyo,Hussein Bashe kunusurika
kutekwa.Tukio hilo lilitokea juzi
usiku wakati Bashe alipokuwa
akitoka ofisini kwake Sinza
Kijiweni, akielekea nyumbani
kwake Mbezi.
Akizungumzia tukio hilo, Bashe
alisema wakati anaondoka
ofisini kwake kwa gari lake,
alianza kufuatiliwa kwa nyuma
na magari mawili, likiwamo aina
ya NOA ambalo hata hivyo
hakufanikiwa kujua lilikuwa na
watu wangapi.
“Kama kawaida nilishinda ofisini
kwa ajili ya majukumu yangu ya
kazi na muda wa kutoka
ulipowadia, niliondoka kurudi
nyumbani.
“Awali wakati navuka geti la pale
ofisini,sikuwa na shaka yoyote,
lakini kadri nilivyozidi kuendelea
na safari yangu, niliona nyuma
nafuatiliwa na magari mawili
ambayo yalikuwa yakiendeshwa
kwa tahadhari.
“Nilipofika Mwenge ile NOA
ilikuwa bado iko nyuma yangu,
sasa nikaanza kupatwa na
wasiwasi, nikajua hapa kuna
jambo.
“Moyoni niliendelea kumuomba
Mungu, huku nikijiuliza maswali
mengi hawa jamaa ni akina nani,
kwa kweli sikupata jibu zuri.
“Nilipofika Mbezi, niliona yale
magari yanazidi kunisogelea,
kwa hiyo,nikaamua kuongeza
kasi na wao wakazidi kuja tu.
“Wakati niko Mbezi jirani na njia
panda ya kwenda kwangu,gari
moja lilinipita kwa kasi na
kuendelea mbele.
“Unajua kuelekea kwangu pale
kuna barabara kama tatu
ambazo zote unaweza kuzitumia
na zikakufikisha hadi nyumbani
kwangu,”.
Alisema Bashe na
kuongeza:
“Nilichokifanya nilipita barabara
ya kwanza na wao wakapita
barabara ya pili na ghafla
nilikutana nao uso kwa uso,
wakati huo naelekea kwangu na
kibaya zaidi,gari lao walizima
taa kubwa na kuacha ndogo.
“Walivyona gari langu,walinipiga
taa kuashiria wanakata kona,
lakini cha ajabu walinifuata
nyuma na hapo nikaanza kujua
sasa nafuatiliwa.
“Nilichokifanya sikwenda
nyumbani moja kwa moja,bali
niliamua kupaki gari kwenye
grosari moja iliyoko jirani na
kwangu.
“Baadaye niliamua kuondoka ili
niwazunguke kwa nyuma
nisome namba za gari lao,lakini
sikufanikiwa kwa sababu taa za
nyuma zilikuwa zimezimwa,”
alisema Bashe.
Kwa mujibu wa Bashe,baadaye
aliingia nyumbani kwake na
kuwakuta wageni ambao alikaa
nao hadi saa sita usiku baada ya
kuwasimulia tukio lilivyokuwa.
“Sasa basi, wakati jamaa zangu
hao wanaondoka kurudi kwao,
walikuta lile gari pale pale njiani,
wakanipigia simu, kwamba lile
gari nililowasimulia
linawafuatilia.
“Nikawaambia wageuze gari lao
ili wasome namba, lakini
hawakufanikiwa hata kidogo
kwa sababu wale jamaa
walishtuka na kuamua kutimua.
“Kwa hiyo, nilichokifanya
nilikwenda pale Polisi Kawe na
kutoa taarifa ambapo nilipewa
RB yenye namba KW/
RB/2899/2013,” Alisema.
Machi 6, mwaka huu, Mhariri
Mtendaji Mkuu wa New Habari
(2006) Ltd, Absalom Kibanda,
alitekwa na kuteswa na watu
wasiofahamika.
Katika tukio hilo, Kibanda
alitobolewa jicho la kushoto,
alipigwa kichwani na kitu
chenye ncha kali na kunyofolewa
kucha.Kwa sasa yuko nchini
Afrika Kusini ambako anaendelea
na matibabu.
SOURCE:
MTANZANIA.
2013 March 30.
No comments:
Post a Comment
‹
›
Home
View web version
No comments:
Post a Comment