Pages

Sunday, June 2, 2013

Breaking News...: Ajali mbaya sana Morogoro Road

 Nilipokuwa naendelea na safari tulikutana na Foleni kubwa sana ambayo nilianza kushangaa nini hiki.
 Ni Zaidi ya Kilometa 5 foleni ya Maroli na mabasi hii ilinistua sana kama unavyoweza kuona.
 Nikafika sehemu iitwayo Bwawani kalibu na Mzani Morogoro nikakuta ajali kubwa kati ya Scania na Fuso.
Scania ilikuwa inaelekea Jijini Dar es salaam na Fuso ikielekea Morogoro Ziligongana uso kwa uso na kusababisha haya uyaonayo katika picha hizi.
 Zilikuwa barabarani ikalazimu zisukumwe pembeni kidogo angalau watu wapite.
 Hili Fuso inasemekana Dereva alipoteza uhai wake hapohapo na Konda ameumia sana sana.

 Kama unavyoweza kuona hapo Hata Uskani hauonekani unaweza pata picha kuwa Dereva anaweza akawa katika hali gani.
 Hiii gari niliyopanda na Team yangu tunaelekea Dodoma kwa Ajili yakuhudhulia Kikao cha Bunge Kesho Asubuhi,
Hii ni Scania iliyogongana na Fuson hiyo waliokuwa humu wako Hospitali kwa matibabu.
Kesho Ntakuwa LIVE Bungeni kushuhudia WIZARA YA SAYANSI na TEKNOLOJIA Ikiwasilishwa.
Hivyo stay Tune Ndugu zangu.

Endelea kufatilia hapa hapa www.peterdafi.blogspot.com

No comments:

Post a Comment