Mnamkumbuka mhariri ABSALOM KIBANDA? AMBAE ALITEKWA NA KUTESWA?, amesema
yafuatayo kuhusu wahusika ambao walimfanyia vitendo hivyo vya kinyama
ambavyo vimempa ulemavu wa kudumu wa jicho lake. Nanukuu;
"Acha niliseme hili jamani pengine moyo wangu utatulia. Mmoja wa watu
walio nishambulia ana fanana kwa sura na umbile la Ludovick Rwezaura
yule kada wa CHADEMA aliyewekwa ndani na Lwakatare ambae nimemuona
kupitia magazeti na mitandao ya kijamii. Nimeshangazwa sana mtu huyu
yupo karibu na baadhi ya wahariri wenzangu na hata msaidizi wangu bwana
Ansbert Ngurumo, bado napata shaka ni kuwa watu wana fanana au?"
My take;
Ndugu Ludovick ambae kwa sasa bado yupo mahabusu, alikuwa ni mfanyakazi
wa CHADEMA makao makuu, chini ya kurugenzi ya ULINZI na USALAMA kabla ya
kukutwa na mkasa wake ambao ndio umemuweka rumande mpaka hivi sasa.
Kuwepo kwa kijana huyu kwenye hii kurugenzi na maelezo ya bwana Kibanda
nadhani wana-JF mnaweza ku-connect dots.
CHADEMA ukweli ni kwamba mwaka 2013 umekuwa mwaka 'tasa' kwenu, kwani
mikakati mingi ya kichama imekuwa ikibuma na mbaya zaidi ni pale mpaka
siri za ndani ya chama kuzagaa mitaani, haya yote ya kubuma na kuvuja
kwa siri ovyo ovyo hivi, kuna sababishwa na 'uchanga' wenu katika
kusimamia shughuli za kichama, mna safari ndefu sana.
Source: DIRA YA MTANZANIA.
No comments:
Post a Comment