Kwa wale waliokuwa wanafuatilia siasa chafu za CCM mkoa na wilaya ya Geita kuhusiana na kuidhoofisha CHADEMA Geita, hatimaye mkakati huo uliowekwa wazi na Mwenyekiti wa ccm mkoa wa geita bwana Kasheku Joseph Msukuma kuwa baada ya kuisambaratisha CHADEMA Kata ya Katoro kwa kumtumia aliyekuwa Diwani wa Katoro kupitia CHADEMA bwana Gervas Daud aliyevuliwa uanachama mwaka Jana, April baada ya kufanya kazi za ccm sasa CCM wanahamia kata ya Kasamwa.
Ni kwamba pale kasamwa kuna eneo la stend ya kata lililokuwa limekaliwa na mganga wa kienyeji aliyekuwa akiwaagulia viongozi wa CCM na serikali ya Geita na hivyo kumilikishwa isivyo halali kukaa eneo llilitakiwa kujengwa stendi ya kasamwa kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote.
Baada ya kupatikana diwani kupitia CHADEMA Wananchi walimuomba Diwani wao kusaidia juhudi za kulirudisha eneo lao la stend toka kwa mchawi huyo wa CCM, Diwani aliitisha Mkutano wa hadhara wa kisheria mwaka 2011 na kueleza azima ya kumtaka mganga huyo wa kienyeji kupisha eneo hilo kwa utaratibu ili wanachi wajenge stendi yao, baada ya mkutano ule Wananchi kwa ghadhabu waliamua kwenda kumtoa mganga yule kwa nguvu kwa kumchomea VILE VINYUMBA VYA KIGANGA ILI AONDOKE. Hapo ndipo kesi ilipoanzia kwa kumkamata Mh. Diwani Mahenge na wananchi baadhi.
Kesi hiyo iliendeshwa tangu 2011 na kukosa ushahidi muhimu na hivyo kuendelea kupigwa tarehe bila mafanikio, baada ya ccm Geita kuonekana wamekabwa sana koo na Diwani huyu machachari sana ndani ya mkoa wa Geita, waliamua kukaa kikao na kufanya mikakati ya kuifufua kesi ya Diwani huyu na kudhamilia kumfunga ili wapumue. Walifanya hivyo na hatimaye mwaka huu mwezi wa april hukumu ilisomwa na Hakimu mfawidhi wa Wilaya ya Geita aliamtia hatiani yeye na wenzake watano kwa kumfunga miaka mitatu (03)
CHADEMA ilifanya juhudi za hali ya juu ya azima ya kukata rufaa na kupata dhamana kwa wafungwa wote sita, baada ya kukaa magereza miezi miwili walipata dhamana na kukubaliwa rufaa. kesi hii ilipata mawakili wawili na iliendelea hadi leo hukumu iliposomwa kwa kuwaachia huru wananchi watano waliokuwa wamefungwa na Mh. Diwani na kumtia hatiani tena yeye eti kwa kuwa yeye ndiye aliyeitisha mkutano ule uliopelekea vijumba vile vya mganga wa kienyeji kuchomwa moto.
Mambo ya kujiuliza ni haya yafuatyo kwa wanaojua sheria:
- Kifungo hiki kimetokea baada ya mkutano wa CCM uliofanyika tarehe 31.08.2013, viwanja vya Kalangalala Geita na Mwkt wa CCM Mkoa wa Geita bwana Msukuma kusema amemaliza kuisambaratisha CHADEMA Katoro kwa kumtumia Diwani mamluki aliyevuliwa uanachama mwaka 2012, sasa anahamia kuimaliza Chadema Kata ya Kasamwa.
- Ni sheria gani aliyotumia Judge wa Mahakama kuu leo Mwanza ya kumtia hatiani Mh. Diwani Mahenge peke yake na kuwaachia wale Wananchi wenzake waliokuwa wamefungwa pamoja eti ni kwa kuwa yeye alikula consipiracy kwa kufanya mkutano uliopelekea wale Wananchi kwenda kuchoma nyumba ile ya Mganga wa kienyeji.
- Je ni sheria gani iliyomwingiza Mh. Diwani Mahenge hatiani kwa kifungo hicho alichopewa kwa kosa la uhalibifu wa mali bila option ya kulipa fidia.
Wadau naomba kuwasilisha."
ALimaliza kwa kusema hivo mwenzangu huyu.
Habari hii nimeikuta Jamii Foram imetumwa na Mtu anaitwa NYAMIGOTA, so naitaji mwenye akili timamu asome vema kisha atwambie nikweli Mahakimu wa Geita wametenda haki9 au Laa.
...................................................................................................................................................................
Lakini hebu tujiulize haya....!!!??
1. CDM kwanini wawe wao tu?
2.CDM kwanini kila wanapofanya mkutano lazima kuna Mauwaji, Vurugu ama maandamano yanayopelekea madhala makubwa kwa wanajamii, jamii au mtu flani?
3.CDM kwani hawawezi kufanya mikutano yakistaarabu tu kama ya CCM?
4. CDM Tumewapa huo Udiwani na Ubunge yanatokea haya yote je tukisema tuwape Uraisi watu siwatakuwa wanachinjana Live?
5. Watanzania tujiulize Kila wanapokuwepo CHADEMA kwanini panakuwa hakuna AMANI wala UPENDO?
6. JE, CDM ni wao tu ndo huwa wanakosewa kwani hakuna vyama vingine vya Siasa Tanzania?
7. Nikweli wanachadema wengi wao hawana Ustaarabu kiasi kwamba wanashindwa kupambanua mambo na kuitunza Amani ya Nchi hii?
7. Je, Nikweli CDM wao ni Muhimu sana zaidi ya hii Tanzania yetu na watanzania?
8. Kwanini CHADEMA wanataka kuwapandia vichwani watanzania?
9. Kwanini wanashindwa kuheshimu Sheria, Taratibu na Misingi ya Nchi hii?
10. Tunawaagiza kama wawakilishi katika vyeo tunavyowapa kwanini hawataki kufanya kazi tuliyowapa badala yake wanabakia kupingana na Serikali, Sheria na Kanuni mbalimbali za nchi na Taasisi ?
11. Kwanini CDM wanautafuta Umaarufu kwa Nguvu?
12. Kwanini CDM wanataka Madaraka kwa Force, Maandamano, Mauwaji, Tindikali, Mapanga , Marungu, Bunduki, Nk......?
13. Kwanini hakuna sera za kijenga na kuleta faida kwa Taifa bali ni ubishani, Lawama, Chuki, Majivuno, na mengine mengi yasiyo na faida kwa watanzania.?
14....... naomba niishie hapo ntaendelea Badae...!!!
No comments:
Post a Comment