Pages

Monday, September 16, 2013

Lowassa:Mawaziri walinitosa,JK akaniunga mkono


Waziri mkuu aliejiuzulu,Edward Lowassa,ametoboa siri kueleza jinsi baadhi ya maamuzi yake yalivyokwamisha na mawaziri wenzake katika awamu ya tatu ya Raisi Benjamini Mkapa.

Lowassa ambae pia ni mbunge wa Monduli,alitoboa siri hiyo jana wakati akizungumzia mradi wa kuvuta maji kutoka ziwa Victoria kwenda mkoani Shinyanga kwa lengo la kukabiliana na tatizo la maji mkoani humo.

Mradi huo ulitekelezwa na serikali wakati Lowassa akiwa waziri wa maji na maendeleo ya mifugo katika serikali ya Raisi Mkapa.Akizungumza wilayani Kahama,Lowassa alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo ulipingwa na mawaziri wengi katika Baraza la mawaziri,lakini ni mawaziri wawili tu ambao waliunga mkono.

Lowassa alitoboa siri hiyo alipokuwa akizungumza katika harambee ya uchangiaji wa shule ya msingi ya kanisa la African Inland(AICT) na kusema kuwa Raisi Mkapa anastahili sifa kutokana na mafanikio ya mradi huo ambao uliunufaisha mkoa wa Shinyanga na mikoa ya jirani.

"Niwapeni siri,nilipendekeza waraka wa kutumia maji ya ziwa Victoria kwa Raisi Mkapa,naye akaniuliza wale wakubwa tutaweza,nikamwambia tutaweza,akauleta katika Baraza la mawaziri,kule mawaziri wote waliupinga kasoro waziri wa Nje wakati huo Raisi Kikwete na rafiki yangu Mohamed Saif Khatibu walioafiki".Alisema Lowassa na kuongeza

"Mzee Mkapa baada ya kusikia mawazo yote akaamua fedha zitolewe"

CHANZO:NIPASHE.

No comments:

Post a Comment