Pages

Thursday, October 17, 2013

NGARA. Mtoto alipuliwa na Bomu

Mtoto mmoja mkaziwa kijiji cha Mumiramila Kata kata ya Bugarama wilaya ya Ngara mkoani Kagera amenusurika kifo na baada ya kulipukiwa na bomu.

Mtoto huyo amejeruhiwa sehemu mbalimbalizamwili wake na amelazwa katika Hospitali ya misheni Rulenge wilayani humo kwaajili ya matibabu.

Mganga wazamu wa hospitali ya Rulenge Bi.Hilda Kagaruki amemtaja mtoto huyo kuwa ni Wema Kigenda (12) ambaye alijeruhiwa na bomu hilo lililomkata miguu miwili na kumtoboa tumbo nakupelekea utumbo wa ndani kutoka nje na kupoteza damu nyingi


na  Pamoja pure

No comments:

Post a Comment