Narudia tena SIIPENDI CHADEMA na sitakuja kuipenda CHADEMA kama haitajirekebisha.
Nasema hivyo kutokana na sababu zifuatazo.
1. CHADEMA imekua inaongoza nchi kinyume na taratibu. Tunajua kwamba kwenye uchaguzi mkuu uliopita CCM "ilishinda" uchaguzi huo na kua na "haki" ya kuongoza serikali na vyombo vyote vya usalama.
Lakini kwa masikitiko makubwa CHADEMA wamejitwalia jukumu hilo bila kufuata sheria na taratibu za nchi hii.
Mfano ni pale CHADEMA inapotumia polisi kuwadhuru wananchi na kuwapiga mabomu wananchi kwa kutumia polisi.
2. CHADEMA kutumia mabavu kuliongoza BUNGE ambapo kisheria ilibidi bunge liongozwe na CCM yenye wabunge wengi, speaker,naibu speaker na wenyeviti wa bunge kutoka CCM.
Hii inajidhihirisha pale ambapo CHADEMA wamekua kimbelembele kutetea maslahi ya wananchi wakati hii kazi ilibidi ifanywe na CCM yenye wabunge wengi+serikali. Huu ni uporaji wa haki ya msingi unaofanywa na chadema kwa wabunge wa ccm.
3. CHADEMA kwa makusudi kabisa imekua ikiwachonganisha wananchi na serikali yao tukufu ya CCM.
Kitendo cha chadema kufichua maovu ya CCM na kuyaweka wazi kwa wananchi ni uchonganishi mkubwa na unawafanya wananchi kutoipenda serikali yao "halali" iliyopo madarakani.
Mfano mzuri ni list of shame, KAGODA, MEREMETA, DEEP GREEN e.t.c
4. Kitendo kiovu kinachofanywa na CHADEMA kuilazimisha CCM kuacha sera zake na kutekeleza sera mbaya za CHADEMA ni kitendo ambacho hakivumiliki na kinafaa kupingwa na wananchi wote. Wanancchi tumekiamini chama chetu tukufu ccm na tukakipa "kura" za kutosha ili kiingie madarakani na kutekeleza sera zake ilizokua inazinadi majukwaani. Matokeo yake CHADEMA imefanya hila na michezo michafu ya kisiasa na kuilazimisha CCM kutekeleza sera za CHADEMA.
5. CHADEMA imeiweka nchi rehani kwa kulazimisha USALAMA WA TAIFA kuripoti kwake badala ya kuripoti kwa serikali tukufu ya CCM.
Huu ni uhaini na wapenda haki wote inabidi tupaze sauti kukemea hili suala.
Haiwezekani wanausalama watiifu wafanye mauaji yanayofuata sheria halafu wale wanausalama wasiofuata maadili wakapeleka taarifa chadema. Hii sio sawa kabisa, kunaiweka nchi yetu kwenye hatari kubwa sana.
Naomba niishie hapa ila natoa rai kwa watu wote wenye uzalendo na nchi hii kuipiga vita CHADEMA kwa nguvu zote.
Pages
▼
No comments:
Post a Comment