Pages

Monday, November 25, 2013

Mbunge ni Mfanyakazi wa Wananchi Kigwangalla Kathibitisha Hilo kwa Kusema haya...!!

Mh, Kigwangalla amekuwa akifanya kazi zake kwa ukaribu sana na wananchi wake na hasa wale wananchi wa kawaida. lakini pia amekuwa mchapa kazi Hodari kwa kupambana uku na uku ilimladi mambo yaende sawa Nchini kwetu.
Kwa sasa yuko Uingereza na amesema hivi........!!!

"Nipo ziara ya kikazi na Kamati yangu nchini Uingereza. Leo mchana saa nane tutakuwa na kikao cha pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Local Government ya Bunge la Uingereza (House of Commons), Mhe. Clive Betts, MP akiwa na wajumbe wa Kamati yake. Tutajifunza kutoka kwao ni namna gani wanafanya kazi ya kuwa jicho la wananchi kwenye kuisimamia na kuishauri serikali juu ya kutekeleza majukumu yake ya kuleta maendeleo ya serikali za mitaa kwenye nchi yao.'


 Lakini pia Hukubali na kuheshimu mawazo na Michango ya wadau mbali mbali, Alisema hivi jioni ya Leo...!!

"Uwakilishi na uongozi si kazi rahisi sana, siyo kazi ya ukosi mweupe (white collar job). Ni kazi ngumu inayohitaji muda, uvumilivu na ubunifu wa hali ya juu. Ni kazi inayotaka mtu ujitoe na uwe tayari kuwahudumia na kuwatumikia wengine. Kila mtu anakutarajia uwe perfect na wote wanasahau kabisa kwamba na wewe ni binadamu kama wao tu, na wanasahau zaidi kuwa kiongozi anatokana na wao. Maisha yangu yote nimekuwa mpambanaji sana na siku zote sikuwahi kukata tamaa na wala kukubali kushindwa. Naendelea kuwaomba wananzega wenzangu mzidi kunisapoti na kunipa ushauri mzuri wa namna bora zaidi ya kuwaongoza kufikia ndoto zetu za jimbo, wilaya, mkoa na Taifa kwa ujumla. Kuwa Mbunge siyo kwamba najua kila kitu. Kuwa msomi siyo kwamba sihitaji elimu. Nahitaji msaada na ninawashukuru watu mbalimbali walioendelea kunisaidia kufanya kazi hii mf. Ndg. Majaliwa Bilali, Ndg. Furaha Titus, Ndg. Godson Kabamba, Ndg. Gisberth Kabamba, Ndg. Eliphace Fredrick Ruangisa, Ndg. Peter Dafi na Ndg. Kajoro Vyohoroka. Msichoke kuendelea kuniunga mkono, muda wangu unakimbia kwa kasi ya ajabu na ahadi kwa wananchi zinahitaji kukamilishwa ili kesho Chama changu kisipate wakati mgumu wa kujibu maswali magumu mbele ya umma."

No comments:

Post a Comment