- Mimi nikiwa Mwana CCM na Kiongozi pia wa CCM ngazi ya Taifa na
Blogger, naomba kusimama mbele ya Mheshimiwa Mbunge Kapuya na Taifa zima
la Tanzania pamoja na wasomaji wangu wote wa Blog na meble ya Mungu,
kukubali makosa na kuomba radhi, kwake na kwa Mungu wangu zaidi. Mimi ni
mmoja wa watu wa kwanza kuamini hadithi iliyojitokeza hivi karibuni
kwamba Mheshimiwa Kapuya amembaka na kumuambukiza Ukimwi na kutishia
kumuua msichana wa miaka 14.
- Leo ninaomba kusimama hapa na kusema kwamba hii habari ni uongo na ni
uzushi wa hali ya juu sana uliotengeenzwa na msichana mzoefu wa uzushi
ambaye kwanza si kweli kwamba ni Mwanafunzi, pili ni Mtumzima mwenye
mtoto tayari hata kabla hajakutana na Mh. Kapuya, pia ni muongo na
mzushi mzoefu aliyewahi kuwadanganya pamoja na Mkurugenzi wa CRDB Bank,
pamoja na kuidanganya TAMWA ambayo iliishia kumuripoti polisi na kuishia
kwake kukaa rumande Segerea kwa muda mrefu sana.
- Kwa nini niliaiamini hii hadithi ni kwamba kuna siku mimi binafsi
tulikuwa tumekaa faragha na Viongozi wengine Watatu wakubwa wa Taifa
ambapo mbunge mmoja aliyedai kuijua kwa undani hii hadithi na kuhusiaka
nayo, alianza kutuelezea hii hadithi kwa kutmia details kubwa kubwa
sana, binafsi nilikuwa ninamuamini sana yule mbunge mpaka leo
nilipothibitisha kwa 100% kwamba hii hadithi haiko sawa either na yeye
ni muongo wa makusudi mwenye nia mbaya na Mh. Kapuya au na yeye
alidanganywa na huyu msichana, ambaye jina lake kamili ni Hamida as
opposed na majina mengi ya uongo ambayo amekuwa akiyatumia kudanganyia
watu.
- Ninaomba kuwa wa kwanza kubeba huu msalaba, najua kwamba sio rahisi
kueleweka na wengi ambao tulishamuhukumu Mh. Kapuya, lakini ukweli ni
kwamba ni hadithi ya kutunga iliyoutngwa na msichana mmoja aliyebobea
katika uzushi na uongo wa hali ya juu sana. Majuzi Waziri mmoja
ninayemuamini sana katika Serikali ya sasa alinishitua kwamba hii
hadithi ni ya uongo niiifuatilie tena, lakini sikuamuamini mpaka leo
asubuhi sana nilipopigia sim na gazeti moja maarufu sana la Udaku,
walioniambia kwamba hii habari si ya kweli na kwamba wanaye huyu
msichana pale ofisini kwao, toka asubuhi mpaka sasa nimekuwa kwenye
uhakiki wa hii ishu, na sasa ninasema wazi na tena kwamba:-
NINAMUOMBA RADHI SANA MH. KAPUYA NA NI MATUMAINI YANGU MAKUBWA SANA
KWAMBA WALE WOTE TULIOHUSIKA NA KUMHUKUMU TUTAKUBALI MAPUNGUFU YETU KAMA
WANADAMU NA KUMUUNGAMIA CHINI MUNGU WETU, NI KWELI MH. KAPUYA ALIKUWA
NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA HUYU BINTI LAKINI YA HIARI SIO KAMA
ILIYOELEZWA NA SI KWELI KWAMBA HUYU BINTI NI MWANAFUNZI, HAPANA ANA
MTOTO TAYARI NA PIA ALISHAWAHI KULIDANGANYA JESHI LA POLISI HUKO NYUMA.
- Wale wote tunahusika na media tujifunze tena na hili fundisho,
tujitahidi kuwa waadilifu na kufanya utafiti wa kina kabla ya kuruka na
hadithi nzito kama hii ambayo inaweza kummaliza mwananchi mwenzetu, au
kiongozi bila sababu za msingi wala ukweli.
- AGAIN NI MATUMAINI YANGU KWAMBA WALE TULIOHUSIKA NA KUMHUKUMU
MHESHIMIWA KAPUYA, TUTAJITOKEZA TENA IN THE PUBLIC NA KUMUOMBA RADHI NA
MSAMAHA.
- MUNGU IBARIKI TANZANIA NA KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!
Imeandikwa na Ndugu W.J. MALECELA (Jamii Forum)
No comments:
Post a Comment