Pages

Thursday, November 21, 2013

NASHANGAA SANA

NASHANGAA SANA.

Hawa ITV na kipindi chao cha MALUMBANO YA HOJA na Baadhi ya Vipindi Kuna Mambo yananishangaza Sana.

1. Hizi Mada za Kila wiki naona Kuna kautaratibu ka Kuziandaa kwakuuliza swali likiwa limeegamia upande Furani!

2. Utaratibu wa Wageni wanaokuja ktk Kipindi Kutokupewa Muda wakutosha Kuelimisha Juu ya Swala Husika,
 Mfano: Leo kulikuwa na Kipindi wakizungumza habari za Mashine za EFD wageni toka TRA, toka katika Kampuni za Wasambazaji Hawajapewa Muda wakujibu maswali waliyoulizwa na wananchi walikaribishwa Studio, Pia kuna Baadhi ya Uzushi umejitokeza ktk Michango ya wananchi, Mtangazaji Kamalizia kwa Kutoa Dakika Moja moja kwa Meza Kuu kutoa majibu, kitu ambacho si sahihi.

3. Watangazaji wamekuwa wakionyesha #Live kuwa anaegemea upande Furani wa Mada kitu ambacho si sahihi kwani Media Ethics haziruhusu mtangazaji kusaport upande wowote.

Kumekuwa na kupewa Muda mrefu kwa watu wanaolalamika zaidi kuliko kwa wanaotoa Maoni au wanaotoa elimu au wanaofafanua ukweli wa Jambo husika Tatizo husika. Hii inapotosha uma na watanzania kwa Ujumla.

Chombo cha Habari chochote kile kina Nguvu sana kwa Jamii kwani Neno moja likisikika, Kusomwa au kuonekana ktk Chombo cha Habari Tambua Neno hilo Litakuwa Limeamsha Morari ya Kujenga au Kubomoa kwa Alielisikia au Kuona hicho.

Hivo Basi nivema Mfumo wautangazaji na Urushaji wa Matangazo ungebadilika kwa Maana yakwamba Pasiwe na Urushwaji wa Mambo yasiyo na Ukweli, Uhakila na Uzushi kupewa Airtime.

Zifuatwe zile Sheria za Utangazaji na Urushaji wa Matangazo kwani tusipofanya ivo Upotoshaji unazidi na tunatengeneza Taifa la Watu wasiojua ukweli bali Uzushi, uongo, na Brabraa...

Tumekuwa Tunapenda sana Kulalamika  na Kutafuta Mtu wakumtwika lawama na kumshutumu kila siku kwa makosa yetu lakini tunayahamisha kwa Mtu, Taasisi au Serikali kitu ambacho si sawa, na Haiwezi kutusaidia , Hii inatokana na Media hazitutangazii Ukweli na Uhakika wa maisha halisi.

Tizama Leo hii kila Taarifa utizamayo kila siku Kama kuna Habari Tano basi Tatu nimigogoro na Mbili ndo habari za Kushawishi au Kutujuza jambo, kitu hiki kinapelekea watanzania kujua kuwa Ugomvi, Kugoma, Kulalama, Kushutumu, Kusemasema, nk.. ndo maisha sahihi ambayo sisi tunapaswa kuishi.

Hii ipo ktk Media Nyingi sana sasaivi hapa kwetu Tanzania, Tubadilishe na Tubadilike kwani tunaalibu Nchi yetu.

#LetsChangeTanzania

No comments:

Post a Comment