Pages

Thursday, November 28, 2013

TAMISEMI kuhitimisha kazi zake kesho ijumaa huko UK...!!

 Amesema Mbuge wa Jimbo la Nzega na Mwenyekiti wa Kati hiyo ya TAMISEMI, amesema Kwamba.

"Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) itahitimisha kazi zake hapa UK kesho Ijumaa Jioni saa 12 kwa kukutana na watanzania wanaoishi huku kwa malengo ya kuzungumza nao ili kubadilishana mawazo, kusikia kero zao, ushauri wao wa namna wanavyoiona Tanzania kutokea huku nje ya nchi na kupendekeza kwa Kamati ni namna gani tufanye ili tuweze kusonga mbele kwa haraka zaidi kama Taifa, pia kamati itapenda kujua kutoka kwao ni namna gani wanaifaidisha nchi wao kama watanzania walioko huku nje ya nchi. Mkutano utafanyikia kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo Ubalozi wa Tanzania UK, pale Tanzania House. Mkutano huu utakuwa ni fursa pia kwa wabunge kujifunza kwa kusikia kutoka kwa wenzetu hawa ili tujue ni namna gani tuishauri serikali kuhusu mambo mbali mbali ya diaspora. Hivyo watanzania wote mlioko UK na nchi jirani mnakaribishwa kufika bila kukosa. Ahsanteni."

No comments:

Post a Comment