Peter Msigwa asema ivi
Shame
kwa Mwigulu nchemba anatuponda chadema halafu hoja yake yote amejenga
kwa kutumia quotation yangu, AKILI NDOGO KUTAWALA AKILI KUBWA,Kama ni
mwuungwana na msomi walau angeninukuu, ,Mwigulu utatuelewa tu,
Kuvuliwa
vyeo kwa Zitto Zuberi Kabwe na Dr Kitila Mkumbo kutakuwa na visingio
vingi, ukweli ni kwamba "NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATAWALA AKILI
KUBWA" It is natural kwamba akili ndogo ikitawala akili kubwa,
1) Yatatumika mabavu na nguvu nyingi kuizuia akili kubwa kupanda juu,
2) Zitatafutwa sababu nyingi na visingizio uchwara kuhalalisha kuizima
akili kubwa tofauti na vigezo vya hoja kwakuwa akili ndogo haiwezi
kuizidi akili kubwa kwa hoja,
3) Hutumika vitisho vingi kuzuia akili kubwa kuchukua hadhi yake
4) Akili ndogo ni rafiki wa akili ndogo mwenzake, hivyo akili ndogo
huzungukwa na akili ndogo kwakuwa ushauri wa akili kubwa akili ndogo
hushindwa kutumia ama kushindwa kuonesha umiliki mbele za watu. Kwenye
chadema wenye akili wote wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo. Pale
bungeni watu wanaoweza kufundisha na waliokuwa wakifundisha hata unaibu
waziri kivuli hawapati kwakuwa wanatumia akili zaidi badala ya nguvu.
Lakini walioishia kidato cha kwanza,
pili, tatu na zero ndio think tanks na ndio majembe ya chadema kwakuwa
wanatumia mabavu na manguvu zaidi kuliko akili sawasawa na matakwa
mahitaji ya akili ndogo inayoongoza akili kubwa. Vijana wahitimu wa vyuo
wanaopenda siasa waliandikiwa barua kuwazuia kuhutubia mkutano wowote
wa hadhara sawasawa na matakwa ya akili ndogo inapotawala akili kubwa.
Zito, Kitila, Christowaja, Matiko, Opulukwa, Baregu, Leticia, Selasini,
Arfi, Akunay, Naste wengi wao MA holders kwa chadema ni rejects. Ukiwa
mwanafamilia au ukoo au kazi au wito maalum wa viongozi ndio utakwepo
kwenye list. I know Zitto tangu tukiwa chuoni, he is a brilliant and
consistent politician, namjua Dr Kitila tangu chuoni, he is resourceful.
Hivi kosa walilofanya ni kubwa kuliko mchango wao waliofanya kwenye
kuwajenga watanzania kuwaamini vijana kwenye siasa? Je kosa lao ni kubwa
kuliko mchango wao unavyohitajika? Vijana tuko kazini na wakati huohuo
tuko mafunzoni. Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye
fursa ya kujifunza zaidi. Haya ndio madhara ya AKILI NDOGO KUTAWALA
AKILI KUBWA, HOFU NDIO HUTAWALA
Peter Msingwa
Wanachama
na wapenzi wa CHADEMA IRINGA naTanzania kwa ujumla, tumefanya maamzi ya
mhimu na yaliyotulazimu kuyafanya kwa faida ya Chama chetu ,na
tutaendelea kufanya Kama ni lazima ili kulinda na kukijenga Chama chetu
kuelekea uchaguzi mkuu. Niseme tu Chadema iko na itakuwa imara zaidi
bila kujali umaarufu wa mtu,tuendele kukijenga na kukiimarisha Chama
chetu. CHADEMA NI BORA ZAIDI KULIKO MTU MMOJA MOJA.HATUTARUHUSU MTU
AFANYE KAZI YA CCM KWA KUTUMIA JUKWAA LA CHADEMA.
Tunawashukuru
watanzania kwa kufuatilia kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Nawapa pole
wote waliokwazwa na jambo hili, na ninawashukuru wote walionipa pole na
kunitia moyo. Ninawashukuru pia walionilaumu na ni vizuri kunyosheana
vidole na kuwekana sawa pale ambapo moja wetu anaonekana kukwamisha
harakati za mabadiliko.
Haya ni mawimbi katika harakati za
mabadiliko na ninaamini yatapita na hayatayumbisha mchakato wa kusimika
mfumo wa demokrasia hapa nchini kwetu.
Ninashauri tuwe na
subira katika kutoa hitimisho na hukumu katika jambo hili. Mpaka sasa
tumekwisha kupata upande mmoja juu ya kilichotokea. Vuteni subira nasi
tuseme ndipo mpitishe hukumu. Mungu akijalia tutakuwa na mkutano na
waandishi wa habari wakati wowote kabla ya wiki ijayo na tutaeleza
upande wetu, na hasa kutoa maoni yetu juu ya kile kilichotamkwa jana
kwamba sisi ni wahaini na wahujumu ndani ya chama chetu.
Kwa
sasa tambueni tu kuwa mie binafsi bado nipo imara katika kuhakikisha
kwamba siwi kikwazo na ninachangia kikamilifu nguvu zangu katika
harakati takatifu za mabadiliko hapa nchini.
No comments:
Post a Comment