Pages

Thursday, December 5, 2013

Jamii Forums' Posts: Uteuzi wa Dr. Asha Rose Migiro kuwa Mbunge na swala la Urais 2015


Katibu wa NEC,Siasa na Uhusianao Wa Kimataifa,Dk Asha-Rose Migiro akimsalimia Mbunge wa Monduli Edward Lowassa

Kauli ya UVCCM Bagamoyo kuwa rais hatatoka kaskazini vipi kwa Lowassa, Migiro na Sumaye?

Wakati ambapo rais amemteua Dr. Asha Rose Migilro kuwa mbunge na hatimaye pengine akateuliwa kuwa waziri, kuna fununu kuwa huenda anaandaliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015. UVCCM Bagamoyo waliwahi kutoa tamko kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015 hatatoka kanda ya kaskazini. Sasa najiuliza Migoro anatoka kaskazini. 
Lakini pia kuna wanaCCM wengine kutoka kaskazini wapo katika kampeni kubwa ya kuwania urais 2015. Hawa ni Edward Lowassa, Fredrick Sumaye na hata Steven Wassira naye nasikia yumo.
 Kauli ile haijawahi kutenguliwa au kukemewa na kiongozi yeyote wa CCM sawa na kauli ya "..wapigwe tu, maana tumechoka sasa..." ya Bwana Mizengo Pinda. Wakati huu wagombea wa CCM kutoka kaskazini wanapozidi kujiimarisha na kuimarishwa katika CCM hali itakuwaje. Maana kaskazini ndiko Nape amekuwa akikipiga vita CHADEMA kuwa kimeegemea kanda hiyo na ukabila kwa kanda hiyo akisahau kuwa hata rais wa kwanza na mwasisi wa CCM marehemu Mwl J. K. Nyerere anatokea kaskazini. Sasa inakuwaje wakati huu harakati za wagombea kupitia CCM zikionekana wazi kuwa kaskazini ina wengi kuliko kanda nyingine na wakati jumuiya imeweka msimamo na Nape akipigilia msumari wa mwisho? Haya yakifanyika kwa CHADEMA wataita ukanda, kwa CCM naona mhubiri mkuu wa udini, ukanda na ukabila Nape yupo kimya.
 Posted by Tulimumu

Mchezo wa SITTA, atafanyiwa LOWASSA

Wengi wenu mnakumbuka jinsi Samuel Sitta alivyopigwa chini na Chama Cha Mapinduzi katika kiti cha uspika kwa kigezo kwamba "huu ni wakati wa wanawake", CCM wakaamua kumpa kiti cha uspika Bibi Makinda na kumtupilia mbali Sitta.

Kutokana kwamba Lowasa amekuwa akipita huku na kule akipiga kampeni zake za chini kwa chini ili apate uraisi 2015 wakati huo huo wapinzani wake karibia wote wanaona hawana uwezo wa kushindana nae wamekuwa wakiandaa mbinu mpya ya kumuandaa Bibi mwingine ambaye ni Asha Rose Migiro. Bibi huyo aliyewahi kufanya kazi na UN na kuonyesha uwezo mdogo katika utendaji na kuliabisha taifa hivi juzi ameteuliwa kuwa mbunge na raisi kama moja ya mkakati ya kumdhohofisha Lowasa.

Siku si nyingi naamini mbibi huyu atateuliwa kuwa waziri na atazidi kuzunguka nchini ili kujiongezea umaarufu na kujitambulisha zaid kwa wananchi wa vijijini.

Swali: je? mwanamke huyu na watu waliyo nyuma yake wataweza kushindana Lowasa?


Posted by FRANCIS MUKANDALA

No comments:

Post a Comment