Pages

Tuesday, January 28, 2014

TEMBO auwa Majangili....!!

Sasa tembo wameamua kujilinda. Juzi, tembo mmoja amewaua majangili wawili waliotaka kumuua. Tukio hilo limetokea katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi-upande wa Kilosa. Mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa Mjangili hayo yalipita kijijini kwao yakielekea hifadhini kwa ajili ya kuua tembo yakiwa na silaha nzito.

Inadaiwa kuwa tembo aliyewaua majangili alijeruhiwa kwa risasi na kujifanya amekufa.Majangili waliposogea kwa ajili ya kutimiza lengo lao la kuchukua nyara,tembo husika alikurupuka na kuanza kuwashambulia majangili hao hadi kuwaua wote wawili.Halafu, akaziponda maiti na kurundika miti katika maiti hizokiasi cha kuzifanya zisionekane.

Mashuhuda waliofika katika eneo la tukio walikuta maiti hizo pamoja na silaha walizokuwa nazo majangili hao. Natoa pongezi kwa tembo wa Mikumi kwa kujilinda. Tembo wote nchini nao waige mfano huo.

Chanzo: Wananchi wanaoishi kandokando ya Mikumi,upande wa Kilosa na Askari Wanyamapori

No comments:

Post a Comment