Katibu mkuu wa CHADEMA,Dr Slaa,akiwa kwenye mkutano wa kumnadi mgombea
ubunge wa chama hicho,jimbo la Kalenga,Grace Tendega,aamua kutoa msimamo
wa chama kuhusu posho za wajumbe wa bunge maalum la katiba mpya,
Ananukuliwa akisema,
"CHADEMA hatutakuwa tayari kwa wajumbe wa bunge maalum la katiba mpya
kuongezewa posho zaidi ya shilingi 300,000/= (laki tatu),kwakuwa hela
hiyo inawatosha kula,kulala na kufanya kazi zao vizuri wakiwa Dodoma.Na
endapo watazidishiwa,kama chama,watazunguka kwa maandamano nchi nzima
kwaajili ya kupinga upandishwaji wa posho hizo.Kupandishwa kwa posho
hizo itakuwa maajabu kwa taifa hili."
Dr Slaa ametoa kauli hiyo jana tarehe 23-04-2014,akiwa jimbo la Kalenga.
Chanzo:- ITV
No comments:
Post a Comment