HATIMAYE WASHINDI WATATU WA MASHINDANO YA KUSAKA VIPAJI VYA UIGIZAJI (TANZANIA MOVIE TALENTS) KWA KANDA YA ZIWA WAPATIKANA JIJINI MWANZA
Janneth Emmanuel (kushoto), Cresenciah Herman (katikati) na Joshua
Wambura Stanslaus ambao ndio washindi wa Shindano la kusaka vipaji vya
kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakiwa
wanaonyesha zawadi zao za pesa taslimu shilingi laki 5 kila mmoja mara
baada ya kutangazwa washindi wa Kanda ya Ziwa.
Shindano
la Kusaka VIpaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie
Talents limemalizika leo kanda ya ziwa, Mkoani Mwanza kwa washindi
watatu kupatikana na kupewa zawadi zao. Washindi hao ni Janneth Emmanuel , Cresenciah Herman na Joshua
Wambura Stanslaus huku binti mwenye umro mdogo kuliko washiriki wote
Emiliana Fidelis mwenye umri wa Miaka 11 aliweza kung'ara kwa kuonyesha
kipaji cha hali ya juu tokea mwanzo hadi Mwisho wa mashindano haya na
kuweza kuvuta hisia za majaji na kupelekea majaji kumtangaza mshindi wa
shindano hili lakini kutokana na Umri wake kuwa ni chini ya kigezo cha
umri uliohitajika hatoweza kwenda Dar Es Salaam Kwaajili ya fainali
lakini majaji hawakumuacha bure walimpatia zawadi za Shilingi laki Moja
kama ishara ya yeye kuwa Mshindi pia.
Baada
ya Mashindano haya kumalizika Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza sasa Zoezi
linahamia Kanda ya Kati Mkoani Dodoma wiki hii ambapo Zoezi zima la
usajili litafanyika kuanzi jumamosi ya tarehe 12 hadi 15 aprili ambapo
pia watatafutwa washindi watatu pia wa kanda ya kati.
Washindi
hawa watatu wataungana na washindi wengine watakaopatikana katika kanda
zingine katika fainali itakauofanyika Mkoani Dar Es Salaam Na mshindi
kupata Zawadi kubwa ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya 15 bora wakiwa mbele ya majaji tayari kwa kuchaguliwa washiriki watano bora.
Hawa ndio washiriki walioingia tano bora
Emiliana
Fidelis akiwa amesimama mbele ya meza ya majaji mara baada ya majaji
kufurahishwa na kuvutiwa na Kipaji chake, Emiliana ni mmoja kati ya
waliotakiwa kuwa mshindi wa Kanda ya ziwa ila kwa bahati mbaya Umri wake
ndio ulikuwa kikwazo.
Jaji
Yvonne Cherry akimkabidhi zawadi ya shilingi laki Moja Mshiriki
Emiliana Fidelis mara baada ya kuvutiwa na Kipaji chake huku akiwa
mshiriki pekee mwenye umri mdogo kuliko wote kwenye mashindano ya Kusaka
Vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents.
Jaji
Mkuu wa Mashindano ya Kusaka vipaji vya kuigiza Tanzania yajulikanayo
kama Tanzania Movie Talents, Roy Sarungi akimkabidhi zawadi mmoja wa
Washindi watatu wa mashindano hayo mara baada ya kutangazwa washindi.
Jaji Single Mtambalike akimpongeza mmoja wa washiriki aliyefanikiwa kuibuka kidedea katika Mashindano ya Tanzania Movie Talents.
Mshiriki
Crensenciah Herman akilia kwa furaha mara baada ya Kutajwa kuwa mmoja
kati ya washindi katika shindano la kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania
lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents lilomalizika Leo Mkoani Mwanza
Majaji
wakiwa katika picha ya Pamoja na washindi watatu wa Kanda ya Ziwa
Mkoani Mwanza mara baada ya Kuwatangaza na kuwakabidhi washindi zawadi
zao.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mwanza
No comments:
Post a Comment