Inawezekana hili likawa moja kati ya maswali uliyonayo na hujawahi
kupata nafasi ya kumuuliza muhusika au inawezekana ikawa ni ishu ambayo
umewahi kuisikia au kuisoma kwenye chombo chochote cha habari.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambae ni mtoto wa Rais wa Jamuhuri
ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwenye exclusive interview na
millardayo.com anasema >>> ‘kuwa mtoto wa Rais changamoto kubwa
ambayo nimeiona mojawapo ni watu kukupa tafsiri ya vitu vingine ambavyo
wewe huvijui, kumekua na malalamiko mengi sana kwamba huyu jamaa ana
mali hizi na hizi’
‘Wanasema kampuni za mafuta, Oil Com, Camel Oil na Lake Oil ni za
kwangu, sasa unajiuliza huyo mtu ambae anaweza akatengeneza kampuni tatu
zinazofanya shughuli moja kwa nini asianzishe kampuni moja ikawa kubwa
zaidi ?? kwa hiyo kumekua na manenomaneno mengi, hizo ni changamoto
mfano kwenye siasa huku, watu wengi aidha hawajui nimetokea wapi au
wanajitoa akili katika maana kwamba hawataki kujua nimetoka wapi’
No comments:
Post a Comment