MWIGULU KATIKA ANGA ZA KIDIPLOMASIA,AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA UINGEREZA.
Kaimu Waziri wa Fedha ndg Mwigulu Nchemba akutana na ujumbe tokea Uingereza. Afafanua mpango na msimamo wa serikali kuhusu mambo ya kiuchumi.
Jana ndg Mwigulu Nchemba ambaye anakaimu ofisi ya Waziri wa Fedha kwa miezi karibu miwili sasa, ameongea na ujumbe wa Iingereza ukiongozwa na Meya wa Jiji la London akiambatana na Balozi wa Uingereza hapa nchini. Katika maelezo yake Kaimu waziri huyu alisema Serikali ina mpango wa kuchukua hatua kadha wa kadha kupunguza urasimu ktk kuvutia uwekezaji ili kukuza ajira kwa vijana.
1) Kuwa na one stop center ktk kukamilisha nyaraka mhimu zinazotoka wizara tofauti. Hivyo kwenye chumba kimoja yaani ofisi moja kuwe na afisa wa ngazi ya juu mwenye maamuzi ili hatua ikikamilika kwa moja iwe imeisha kwa wote kuliko kutoka Wizara ya ardhi unakwenda TIC, unatoka huko unakwenda viwanda, ukitoka huko uende uhamiaji ukitoka huko uende Wizara ya Kazi ukitoka huko uende Uwekezaji na Uwezeshaji, utoke huko uende mipango. Hii inatengeneza urasimu na kujenga mazingira ya rushwa.
2) Pili kuwa na bei za wazi katika rasilimali gesi inayokwenda viwandani ili anayetaka awekeze kwa bei ya gesi ya Taifa badala ya kutegemea makubaliano ya timu ndogo tu kuamua kwa niaba ya watanzania. Hii inatengeneza mazingira ya rushwa. Bei ikijulikana insondoa urasimu na uwrzekano wa rushwa. Bei kujulikana kuna saidia kuweka uwazi na kuwa na mikataba yenye tija kwa taifa
Katika hayua nyingine ndg Mwigulu aliendeleza uzalendo wake wa kutokuwa na uoga kutetea maslahi ya taifa pale alopowambia ugeni bila uoga akijibu maswali yao walipouliza kuhusu mazungumzo yaliyovunjika
1) Uingereza ni Taifa kubwa ni sawa, lakini tunapopatana (Negotiate) kuhusu mikataba msiweke mashariti kuwa bila Tanzania kukubali baadhi ya mambo mazungumzo yanaisha. " With all respect to UK, Tanzania is willing to corporate with UK, But be reminded that we have national interest to be safeguarded everytime, thus as we negotiate do not single out some items and state that without them all negotiations comes to an end. Negotiation has a give and take aspects, in addition there some issues we can not surrender them to make sure publics interests are alwsys observed.
2) Misamaha ya kodi sio kivutio pekee cha uwekezaji kwani tunahitaji kuweka miundombinu kuvutia wawekeji mfano maji, umeme. Hatuwi kutoza kodi kwa masikini na kumsamehe tajiri halafu tutumie kodi ya masikini kumpelekea tajiri,maji, barabara, umeme kwa kodi za masikini.
Masikini wetu akitaka kuanzisha biashara anatoza kodi kabla hajamaliza kufungua biashara, hana tax holday, hivyo ni lazima kodi itozwe ili kuweka sawa maxingira ya biashara. Sio kuwatoza masikini na kuwasame matajiri.
No comments:
Post a Comment