Pages

Saturday, October 25, 2014

KWANINI NITAMUUNGA MKONO DK HAMISI KIGWANGALLA MWENYEKITI WA TAMISEMI URAIS 2015

Kwa nini nitamuunga mkono Dr. Hamisi Kigwangalla, Mwenyekiti wa Kamati ya TAMISEMI Urais, 2015?

(sababu zangu 10).                                                         
1. Ni kijana msomi, anayejitambua na mwenye uelewa mpana. Dr. Hamisi Kigwangalla, MB, ana elimu ya digrii tatu, MD, MPH na MBA (Oganaizesheni na Uongozi) na anamalizia tasnifu yake kwenye PhD (Afya na Uchumi). Mpaka sasa hakuna mgombea anayemfikia kwa kiwango cha elimu. Na pia amesoma elimu kwa upana na kwa urefu, hivyo ana uelewa mpana kwenye mambo meng (multi-skilled).                                
2. Akiwa Rais wa serikali ya wanafunzi, alipata fursa ya kujifunza mambo mengi ya uongozi kutokana na kuhudhuria vikao mbalimbali vya kufanya maamuzi, kama vile Bodi ya Utawala ya Muhimbili, Baraza Kuu la Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Seneti ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam na zaidi.                                                                                        3. Akiwa Chuo Kikuu pia alikuwa mbunifu sana kiasi cha kuanzisha harakati nyingi kwenye jumuiya za wanafunzi vyuo vikuu kwa mafanikio makubwa. Nyingi zikiwa kushiriki shughuli za usafi na kuelimisha kuhusu afya kwenye jamii, kuhamasisha mabadiliko ya tabia ili kupambana na maambukizi ya VVU chuo kikuu - harakati zilizompelekea kupata fursa ya kusafiri nchi mbalimbali kuwasilisha pepa za kisomi kuhusiana na harakati hizo kwenye mikutano mikubwa iliyohusu VVU/UKIMWI na pia kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza wa taasisi ya vijana wenye kupambana na UKIMWI duniani.                                                              
4. Ni mwanaharakati wa kupambana na umaskini kwa vitendo. Ameweza kuhamasisha ufufuaji wa kilimo cha zao la Pamba Nzega na kufanikiwa kukuza uzalishaji kutoka Kg 20,000 mwaka wa kwanza hadi zaidi ya kilo milioni nane, mwaka wa nne wa mradi.
                      
5. Ni mwanaharakati wa kulinda na kutetea maslahi ya wanyonge na wasio na sauti. Amekuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wachimbaji wadogo wadogo nchini, mama ntilie, bodaboda, wamachinga, wakulima, wafugaji na wavuvi. Pia ni mtetezi namba moja wa vijana na amepigana sana vijana wapewe fursa za kuzalisha ajira kupitia kujiajiri kwa kuwezeshwa na serikali kwa maksudi, maana kibaiolojia vijana wanatarajiwa kuishi miaka mingi kuliko wazee hivyo tukiwekeza kwao tutajenga uchumi imara.                                          
6. Amekuwa mstari wa mbele kusema ukweli na kutetea raslimali za nchi kama madini na gesi, akidai zifaidishe wazawa na Taifa la kesho, kama alivyokuwa akielekeza baba wa Taifa.                                                                            
7. Ni mzalendo anayechukia rushwa na ubadhirifu na anayetamani kuona uwajibikaji wa serikali kwa wananchi, nidhamu ya kazi na motisha kwa wanaojitoa kwa ajili ya nchi yetu mfano waalimu, madaktari, maaskari n.k.                          
8. Ni mjasiriamali aliyeweza kupigana na umaskini wake binafsi na wa wapiga kura wake (kupitia kuhamasisha kilimo cha mazao ya pamba na alizeti, kuanzisha na kuwezesha SACCOs na vikundi vya biashara) kwa njia halali. Amefanikiwa kuanzisha biashara na kukuza mtaji wa kampuni zake mpaka zaidi ya bilioni kumi za kitanzania. Tanzania ya leo inahitaji mchapa kazi mwenye uwezo na moyo wa kujituma wa namna hii, pia mtu anayeelewa biashara kwa vitendo. Vijana wanahitaji kuwezeshwa kuzalisha ajira siyo kutafuta ajira. Hakuna mgombea hata mmoja mwenye uzoefu kama huu wa Dr. Kigwangalla.                                
9. Dr. Kigwangalla ni mgombea mdogo kuliko wote mpaka sasa. Ni wa kizazi cha kompyuta na tunatarajia fikra mpya na za kisasa. Ni mwanasayansi, tunatarajia ubunifu, utafiti na matumizi ya teknolojia zaidi.                
10. Amewahi kuwa Daktari wa Tiba Daraja la Pili, Mtaalamu mshauri kwenye afya ya jamii, Mtaalamu mshauri kwenye mawasiliano kwa umma, Mtafiti, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Peercorps Trust Fund, Afisa Mtendaji Mkuu wa MSK Group, Mjumbe wa Bodi mbali mbali; na kwa sasa ni Mbunge wa jimbo la Nzega na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI.
Pia ni Mwenyekiti wa Bodi za makampuni ya MSK Group, Emergent Africa Ltd

No comments:

Post a Comment