Kufuatia kujiuzulu kwa Prof SOSPETER MUHONGO ambaye watanzania wengi walikuwa na imani naye hasa kutokana na juhudi zake za kuwapelekea umeme vijijini tena kwa bei nafuu, kumezuka malumbano huku mitaani kuwa huu ni mpango mkakati wa UKAWA kwa kutumia watu wenye pesa zao hususani wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wana CCM wote ambao wanaonekana kukipaisha chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuchapa kazi wanaundiwa mizengwe ili chama kionekane hakina watu wasafi. Itakumbukwa kuwa wakati sakata la ESCROW linaendelea kumwandama mmoja wa wana CCM mahiri, prof Muongo, mizengwe mingine imeendelea kuibuliwa dhidi ya Majembe ya Chama chenu ilimradi tu kuwaaminisha wananchi kuwa nao si wasafi kama ambavyo walikuwa wamempatia prof. Sina haja ya kuwataja watu ambao wameanza kuchafuliwa kupitia majukwaa ya siasa, mitandao ya kijamii na hata kwenye vikao vya siri.Mpango huu ambao inasemekana una baraka za watu wenye pesa zao kwa maana ya kuuwezesha kwa hali mali umefanya baadhi ya wabunge wa CCM kuingizwa mkenge na kujikuta kupumbazwa na kile kinachodaiwa ni mgawao wanaoupata pamoja na kusifiwa kuwa wao ndiyo wasafi kwenye vikao vya siri wanavyoalikwa.
Lengo la mkakati huu ni UKAWA kuhakikisha wanakwenda kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba wakiwa na agenda moja kuwa NDANI YA CCM hakuna msafi ambapo watakuwa wakitolea mfano watu ambao CCM ilijivunia kuwa wachapakazi lakini wameboronga kwa vile wote watakuwa wamekwisha wapaka matope kupitia huu mpango mkakati.
mytake: CCM mnapaswa kuchukua hatua zifuatazo kuhakikisha mnawalinda watu hawa wanaomulikwa na UKAWA:
1. Waelezeni wabunge wenu kinachoendelea, na kuepuka kutumiwa kuwahujumu watendaji wazuri wa Chama ambao ni tegemeo la Watanzania. Rais bora lazima atoke ndani ya CCM -Nyerere, nami naamini hivyo
2. Nendeni kwa wananchi waambieni wajihadhari na maneno ya kuwachafua watu hawa.
3.Watahadharisheni Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kujiingiza katika mijadala ya kuwamini maneno ya kuwachafua wale wote wanaoonekana kukipaisha chama na ambao tayari wameshaonekana ni mwiba kwa UKAWA.
4. Watahadharisheni Watu wasafi ndani ya chama chenu kutokubali kirahisi kuingizwa mkenge katika kashfa ambazo zinaweza kuwaondolea sifa za kupeperusha bendera ya chama katika nyadhifa mbalimbali katika uchaguzi mkuu ujao.
CCM kama mlikuwa hamjashtukia mambo hayo, basi na mshtuke sasa, hili la Muhongo liwe somo kwenu, mmempoteza mtu muhimu sana kwa sababu tu Mpango ulioandaliwa kukidhoofisha chama pasi kujitambua.
Lakini pia Muhongo kashulkiwa Kwa kuwa Alikuwa anaifanya Kazi yake Kwa Umakini pasipo kuruhusu Siasa wala Magumashi yoyote.
Waliochukizwa wamechukizwa kwakuwa Kuna Maslahi Feki ameyadhibiti kwao kupitia usanii waliokuwanao Wizara ya Nishati Na Madini.
Tusipochanganya Akili Vema Tutakuwa tunaondoa Watendaji Na Kuruhusu Wanasiasa Wafanye Siasa uku Tunaalibu Nchi hii.
*JF
No comments:
Post a Comment