Pages

Wednesday, June 24, 2015

Ripoti ya haki za binadamu kibiashara yazinduliwa

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC leo kimezindua ripoti ya haki za binadamu katika uchumi kwa mwaka 2014 ambayo inaonesha ukikwaji mkubwa wa haki hizo nchini Tanzania.
Dkt Hellen Kijo Bisimba - Mkurugenzi mkuu LHRC
Ripoti mpya imeonyesha kuwa kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika shughuli za uchumi na biashara nchini Tanzania, kiasi cha kusababisha maendeleo katika jamii nyingi nchini kuwa ya chini.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ndicho kilichotoa ripoti hiyo ambapo kwa mujibu wa mratibu wa dawati la uchumi na mazingira la kituo hicho Bi. Flaviana Charles, ukiukwaji mkubwa upo katika sekta za ardhi na kodi.
Bi. Flaviana amefafanua kuwa katika ardhi, wawekezaji wakubwa wamekuwa wakimilikishwa ardhi kinyume na taratibu kiasi cha kusababisha migogoro isiyo ya lazima katika maeneo mengi nchini huku makampuni nayo yakituhumiwa kujihusisha na udanganyifu pamoja na ukwepaji wa kodi.

Chanzo: EATV

No comments:

Post a Comment