Pages

Thursday, December 10, 2015

SERIKALI: TUTALINDA HAKI ZA BINADAMU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiingia katika ukumbi wa Karimjee wakati wa maadhimisho ya Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akihutubia wadau mbalimbali hawapo pichani wakati wa maadhimisho ya Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu akipeana mkono na  mhutimu wa Chuo Kikuu Mzumbe mara baada ya kutoa burudani fupi wakati wa maadhimisho ya Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipokea maandamano katika Ukumbi wa Karimjee yaliyofanywa na wadau mbalimbali wa Haki za Binadamu wakati wa maadhimisho hayo Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Bendi ya Askari magereza waliobeba bango lenye ujumbe wa siku ya maadhimisho ya haki za Binadamu Duniani wakiwa katika maandamano yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.

Kikosi cha Bendi ya Askari magereza wakiongoza maandamano kwa ajili ya kuadhimisha siku ya haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali wakiwa katika maandamano kwa ajili ya kuadhimisha siku ya haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Wananfunzi waliobeba mabango yakiwa na ujumbe mbalimbali unaosisitiza haki za Binadamu zizingatiwe wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa(UN) wakiwa na wadau mbalimbali katika maandamano ya kuadhimisha siku ya Haki za Binadamu  duniani yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
PICHA ZOTE NA ALLY DAUD - MAELEZO.

Na Shamimu Nyaki _Maelezo.
 SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itahakikisha Haki Za Binadamu zinalindwa na kuheshimiwa na kila mtu katika jamii anayotoka bila kujali itikadi yoyote ili kuleta usawa na uhuru katika jamii.

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Haki za Binaadamu yaliyofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijin Dar es Salaamu, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema atahakikisha anasimamia uhuru na haki kwa wananchi wote kwakuwa binaadamu wote ni sawa na wote wana haki sawa.

Mhe Samia ameongeza kuwa Serikali itahakikisha  inakomesha mauaji ya albino,ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na wasichana, ndoa za utotoni,ukeketaji pamoja na mateso kwa mahabusu kwa vile wote ni Binadamu na wana Haki sawa.

Aidha amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoridhia mikataba mbalimbali inayohusu Haki za Binadamu kama vile Mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi wa mwaka 1965, Mkataba wa kuondoa Ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya wanawake wa mwaka 1979 na Mkataba wa kimataifa wa haki za watoto wa mwaka 1989.

“Serikali yetu imekwisha ingiza baadhi ya mikataba hii katika sharia zetu za nchi,ama kwa kuunda sharia mpya au kurekebisha zile zilizopo”Alisema Mhe Samia.

Awali Mkurugenzi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw Bahame Tom Nyanduga katika hotuba yake  amesema kuwa Tume ya Haki za Binaadamu imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa elimu kuhusu haki za binaamu kwa wananchi wote japokua kuna changamoto ndogo ndogo kwa maeneo ya vijijini na wanaendelea na jitihada za kuwafikia wananchi hao.

“Haki na Wajibu ni vitu vinavyoambatana hivyo watu wote washiriki. “Alisema Bw Bahame.
Ameongeza kuwa ni lazima Haki za Binaadamu zilindwe na kuheshimiwa ili kuleta maendeleo katika uchumi wa jamii kwa ujumla kwa kuwa bila  Uhuru na Haki watu watakosa elimu bora,maji safi,uhuru wa kupata habari,kwa kuzingatia kuwa binadamu wote wamezaliwa huru na ni sawa.

Maadhimisho hayo  ni ya 67 tangu yalipoanzishwa  na Azimio la  Ulimwengu la Haki za Binaadamu Mwaka 1948 yamehudhuriwa na watu mbalimbali kutoka Serikalini,Umoja wa Mataifa,Wadau wa Haki za Biadamu, na wanachi kwa  ujumla ambapo kauli mbiu inasema “Haki Zetu,Uhuru Wetu Daima”.

Hata hivyo Tume ya Haki za Binadamu imedhamiria kuleta maendeleo chanya kupitia Mpango wa Maendeleo endelevu utakaonza januari mwakani ambao umekuja na malengo kumi na saba ikiwemo elimu bora,afya bora, pamoja na kuondoa umaskini ili kufikia malengo ya Millenia.

No comments:

Post a Comment