BARUA YA WAZI KWA RAIS.
Mheshimiwa Rais, kwa heshima kubwa tunaandika barua hii kwa hisia kali tukiamini nawe unaudhiwa na watu wachache wanaoidhalilisha na kuichafua sifa nzuri ya Taifa letu kwa makusudi kwa faida zao binafsi na makundi yao.
Mheshimiwa Rais ikumbukwe kuwa Octobar, 25 mwaka 2015 nchi yetu ilifanya uchaguzi mkuu ambao kwa upande wa Zanzibar ulikuwa na kasoro mbalimbali zilizopelekea tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuufuta uchaguzi huo na matokeo yake kisheria.
Mheshimiwa Rais tunaamini kuwa tume ya uchaguzi ya Zanzibar ndio yenye Mamlaka na dhamana ya kupanga, kuandaa, kutangaza ama kufuta matokeo ya uchaguzi bila kuingiliwa na chombo chochote kisheria na kikatiba.
Mheshimiwa Rais licha ya kuwepo kwa uhuru wa kujieleza je ni halali mtu mmoja kwa kutumia kikundi cha watu wachache tunaowafahamu kwa majina kuwaachia kuchafua sifa nzuri ya nchi yetu ndani na nje ya nchi?
Mheshimiwa Rais, je Maandamano tuliyoyashuhudia mwezi Desembar mwaka 2015 na Januari mwaka huu yakifanyika nchini Uingereza,Marekani Sweden Norway na Somalia na watu wanaojiita watanzania, Serikali chini ya uongozi wako ilichukua hatua gani dhidi yao?
Mheshimiwa Rais, pia timu hiyo hiyo imeandaa watu nchini Canada ili kufanya maandamano siku ya Jumatano Januar 27 mwaka 2016, yanayoandaliwa na kuratibiwa na Abdallah Shaib mwenye namba za simu 647-761-5329, Maalim Salim Seif mwenye namba 416-856-4513 na Ndg Zamil mwenye namba 416-826-3361 kuishinikiza serikali kumtangaza maalim Seif Sharrif Hamad kuwa rais wa Zanzibar.
Mheshimiwa Rais maandamano hayo yamepangwa kukutana na kuanzia Jane/Finch Mall saa tisa alfajiri kuamkia siku ya maandamano.
Mheshimiwa Rais, kwa uchungu hatupo tayari kuona watu wachache wakiandaa mikakati ya kuchafua sifa ya Zanzibar kwa uchu wa madaraka huku Serikali ikiwa kimya bila kuchukua hatua yoyote.
Mheshimiwa Rais, Tanzania inabalozi katika nchi hizo zinazotumiwa kuchafua sifa ya Taifa letu je balozi hizo zimechukua hatua gani ili kukabilina na hali hiyo?
Mheshimiwa Rais, je Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ina watumishi wafanyao kazi nje ya nchi ambao baadhi yao ni wanadipromasia, na kwa kuwa sifa na uwezo wao ni kuchambua matukio na kutabiri kinachoweza kutokea tunaamini vibali vya maandamano nje ya nchi vinatoka kwa kuwa Tanzania ni nchi mojawapo yenye kuheshimu haki za binadamu na utawala bora.
Lakini mheshimiwa Rais kwa busara zako huoni kuendelea kutolewa kwa vibali hivyo kwa watu ambao sio Wazalendo na baadhi yao walikimbia na kuukana Utanzania kufanya hivyo ni kuchafua haiba ya nchi yetu katika ulimwengu wa Kidipromasia?
Na je Mheshimiwa Rais huoni kama hilo likiendelea kufanyika ni Kuudhoofisha Uhusiano na Ushirikiano katika sekta mbalimbali na kuiaminisha dunia kuwa Tanzania ni nchi yenye siasa chafu?
Mheshimiwa Rais, Je huoni kufanya hivyo ni kuwapa nguvu maadui wa Tanzania kuwatumia watu hao katika kuwashawishi ndugu zao wa Tanzania ili kuvunja Tunu ya Amani yetu tuliyonayo?
Mheshimiwa Rais, Je huoni kuendelea kufanya hivyo ni kukiuka amri ya Serikali ambayo tayari imetolea ufafanuzi juu ya mkwamo huo wa kisiasa mbele ya wananchi na balozi mbalimbali siku ya maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar?
Katika taarifa hiyo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein alisema ''Napenda niwahakikishie wananchi wote kuwa Serikali zetu zote mbili zitaendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuhakikisha Amani, Utulivu na Usalama vinaendelea kudumishwa nchini.
Nchi yetu inaongozwa kwa katiba na sheria hivyo hakuna Mtu au Taasisi yoyote iliyo juu ya katiba na sheria. Kwa mnasaba huo, swala la kutii sheria na katiba ya nchi halina Mbadala wala Mjadala''.
Mheshimiwa Rais, hatutaki wala hatutavumilia kuona watu wachache wakivuruga amani ya nchi yetu pamoja na kuchafua sifa nzuri ya nchi yetu ndani na nje huku viongozi tuliowaamini na kuwachagua mkiwa kimya.
Kwa heshima kubwa na kwa uchungu tunakuomba Mmeshimiwa Rais chukua hatua kwa watu wachache wanaochafua sifa huku Wazanzibari tuliowengi ambao ni wapiga kura halali tukiumia kuona watu wachache wakichafua sifa ya nchi yetu na Serikali ikiwa kimya.
Mheshimiwa Rais, sisi wananchi wa Zanzibar tunaiomba serikali yako kupitia balozi zake na taasisi nyingine chukua hatua ili kukomesha uchafu huo ili nchi yetu ambayo wazee wetu walipoteza maisha kwa kuikomboa iendelee kuwa salama sambamba na amani iliyopo iendelee kudumu milele.
Nimatumaini yetu kuwa ujumbe wetu utazingatiwa na kufanyiwa kazi kwa mafanikio.
Wako katika ujenzi wa Taifa
No comments:
Post a Comment