Pages

Thursday, January 21, 2016

Mbunge Seif Gulamali aanza kazi yakuwatumikia wana Manonga kwa Kasi kubwa

Gulamali aanza kazi kwa kishindo jimboni Manonga

Mbunge wa jimbo la Manonga wilayani Igunga mkoani Tabora Bw. Seif Khamis Gulamali (CCM) ameanza kazi za kuwatumikia wananchi wake kwa kushiriki ujenzi wa wa vyoo pamoja na kuziba mabwawa yaliyoharibiwa vibaya na mvua.

Mbunge wa Jimbo la Manonga wilayani Igunga Mkoani Tabora Bwn.Seif Khamis Gulamali


Gulamali ameziba bwawa la Maguliati katika kata ya Ziba na kutengeneza mitaro ya maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wa zao la mpunga linalotegemewa na wakazi zaidi ya 600 katika kata ya Choma, pamoja na kushiriki ujenzi wa choo katika shule ya msingi Njia Panda kata ya Nkinga.

Mbunge huyo aliyeshinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana kwa kura 31,485 sawa na asilimia 67.65% alianza kwa kuwashukuru wananchi wake kwa kuzunguka katika kata zote 19 na kuanzisha ligi ya mpira katika vijiji 68 na kutoa jezi pamoja na mipira kwa kila kijiji.

Aidha Gulamali amewaomba wananchi wake kuonesha ushirikiano wa hali ya juu ili aweze kutekeleza vyema kazi waliyomtuma ya uwakilishi na watarajie mabadiliko na maendeleo makubwa katika jimbo lao.


Na EATV News

No comments:

Post a Comment