Pages

Monday, January 4, 2016

Watumishi wa Kada za Afya watakiwa kufuata Maadili na Viapo vya Taaluma Zao

WATUMISHI WA KADA ZA AFYA WATAKIWA KUFUATA MAADILI NA VIAPO VYA TAALUMA ZAO

Geita, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh Ummy Mwalimu aendelea na Ziara Geita.
Mh Ummy Mwalimu Amewaagiza watumishi wote wa Kada za Afya nchini kufanya kazi zao kwa kufuata maadili na viapo vya taaluma zao.
Ameyasema hayo Waziri Ummy alipokuwa Hospitali teule ya Mkoa wa Geita, alipokuwa pale aliambatana na Mganga mfawidhi wa Mkoa wa geita Dkt Adam Sijaona ambae alikuwa akimfahamisha mazingira nakumuelezea changamoto wanazokutana nazo hospitalini hapo.

Pia waziri alitembelea Wodi mbalimbali nakukutana na wauguzi wa Wodi yakinamama, akawasikiliza pia ili kutatua kero zao Hospitalini hapo.

Alipata kuzungumza na Wagonjwa pia katika Wodi hiyo yakina mama nakuwauliza juu ya Huduma wanavyoziona punde wanapo pokelewa Hospitalini hapo, kama zinalidhisha na wanatamani nini kiongezwe ama kupunguzwa.

Lakini Baada ya Hapo Waziri ameelekea ktk Kituo cha Afya Nyankumbu nakusalimiana na wagonjwa  pia kusikiliza changamoto zao na maoni yao ili kuboresha huduma za  Afya Nchini.

Waziri Ummy Mwalimu amezungumza na Tabibu wa kituo cha Afya Nyankumbu mara tu baada yakufika katika Kituo hicho Waziri aliingia katika chumba cha kutolea huduma ambapo alikuta huduma zinaendelea.

Mganga mfawidhi wa hospitali teule ya mkoa wa Geita Dkt.Adam Sijaona akimdadavulia jambo waziri Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea hospitali hiyo
Waziri akimjulia Hali mama aliyejifungua kwenye wodi ya wazazi hospitali teule ya rufaa ya mkoa wa geita

Waziri Ummy akiongea na Wagonjwa waliopanga Foleni kungoja Huduma katika Kituo cha Afya Nyankumbu.
Wauguzi wa wodi ya akinamama katika hospitali teule ya mkoa wa geita

No comments:

Post a Comment