Pages

Monday, February 15, 2016

Maofisa wanne wa MSD Wasimamishwa kazi na Waziri Ummy kwa Tuhumuma za upotevu wa 1.5Billioni

Waziri wa.afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto awasimamisha kazi watendaji wanne wa bohari ya dawa(MSD).

Waziri ummy mwalimu amewasimamisha kazi watendaji hao wakati akipokea vitanda pamoja na magodoro kwa ajili ya akina mama wajawazito toka MSD kwa ajili ya hospitali ya taifa ya muhimbili kwenye wodi ambayo ilikua ofisi ya wizara ya afya Jengo la uzazi wa mama na mtoto ambalo mwishoni mwa wiki Mh rais wa jamhuri ya muungano wa tangania aliagiza wahamishe na litumike kama.wodi

Maafisa hao wamesimamishwa kupitia Ukiukwaji wa kanuni za manunuzi  na hivyo kupelekea ubadhirifu wa takribani 1.5 bn za manunuzi ya dawa na vifaa tiba kati ya 2012 na 2015. Hawa ni:

Waliosimamishwa ni..

1. Bw Cosmas Mwaifwani Mkurugenzi wa Kanda na Huduma kwa Wateja (ambae alikuwa Kaimu Mkurugenzi 2012 - 2015

2. Joseph Tesha - Mkurugenzi wa Fedha na Mipango

3.Missanga Muja - Mkurugenzi wa Ugavi

4. Heri Mchunga , Mkurugenzi wa Manunuzi
Akiongea na Peter Dafi Blog Mh Waziri wa Afya alisema
"Nimeamuru Bodi iwasimamishe kazi ili kupisha uchunguzi wa Upotevu wa Pesa hizo....."

No comments:

Post a Comment