Mkurugenzi wa manispaa ya ilala Isaya Mgulumi(mwenye miwani) akiwaeleza mawaziri wa wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,Ummy Mwalimu(katikati) na waziri was kilimo na mifugo, Mwigulu Nchemba(kushoto) akiwaelezea hali ya ukarabati wa machinjio hayo
Waziri Mwigulu Nchemba akiongea na Umoja huo na kuwapatia siku tatu ili waendelee na uchinjaji wa ng'ombe walizonazo na baada ya hapo wataendelea na ukarabati wakati huo machinjio ya mazizini yatakua yamekamilisha ukarabati na kufunguliwa
Wanachama wa Umoja wa wafanyabiashara hao waliwasikikiliza mawaziri hao
Mbunge wa jimbo la segerea Bona Kalua,akiongea na wanachama wa Umoja wa Wafanyabiasha wa ng'ombe na mazao yake(UWAMI) kwenye mkutano wa pamoja na mawaziri hao
Mawaziri wakisoma vielelezo vilivyowasilishwa na diwani wa kata hiyo
Mkaguzi toka TFDA dkt. Mwanga Itikija(mwenye shati la pink)akiwaonesha mawaziri hao eneo ambalo lilikua likiuzia nyama kwa reja reja kinyume na kanuni ya afya
Baadhi ya wafanyabiashara wa machinjio hayo wakifuatilia ziara hiyo
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na Wanachama wa umoja huo,ambapo.aliwasisitiza kufanya biashara kwa kuzingatia kanuni za afya na kumlinda mlaji hivyo kuwa makini na utunzaji wa mazingira pamoja na mazao wanayoyauza machinjioni hapo
Naibu Meya wa manispaa ya ilaya ambaye ndio Diwani wa kata ya vingunguti Omary Kumbilamoto akiongea kwenye mkutano huo
No comments:
Post a Comment