Dodoma.
Waziri Ummy Mwalimu aadhimisha siku ya Malaria Duniani kwa Kupima Malaria kwa kutumia kipimo cha haraka(mRDT)
Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akiwaonesha waandishi wa habari kipimo cha haraka cha kupima malaria(mRDT) wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya malaria Duniani leo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma
Pichani, Kulia ni mkuu wa kitengo cha udhibiti wa mmbu waenezao malaria charles dismas kutoka mpango wa Taifa wa kudhibiti malaria
Fundi sanifu maabara Habiba Malima akimchukua damu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto kwa kipimo cha malaria Rapid Diagnosist Test(mRDT),kipimo hicho ni cha haraka na huchukua dakika ishirini kugundua kama una malaria,kipimo hiki kilianza kutumika nchini mwaka 2009
Baadhi ya wataalam wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa dodoma pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza waziri Ummy Mwalimu
Afisa habari wa idara ya habari Maelezo eutel Mangi akipima malaria kwa kipimo cha mRDT
Mwandishi wa habari kutoka clouds media Kijah Yunus akipima malaria
Waandishi wa habari wakiwa wamejipanga mstari tayari kwa kupima malaria
Mwandishi wa habari na mmiliki wa globu ya mzee wa matukio richard mwaikenda akichukuliwa kipimo cha malaria na fundi sanifu maabara Habiba Malima
Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria,Dkt.Renata Mandike(kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusiana na utekelezaji wa udhibiti wa malaria nchini
No comments:
Post a Comment