MWIGULU NCHEMBA AWAONYA MADREVA WANAOACHA MAGOGO,MAWE NA MATAWI YA MITI KWENYE BARABARA.
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba akemea madereva wanaoacha mawe na magogo barabarani baada ya kutengeneza magari yao
Aagiza wakamatwe kila wanapobainika kufanya kosa hilo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amekemea vikali jambo hilo kwakati wa kikao cha Bodi ya barabara mkoa wa Singida kilichokaa jana tar 22.11.2016.
Akiongea wa masikitiko,Mwigulu amesema tabia hii imeshamiri kwa baadhi ya madereva kuweka mawe makubwa, magogo au matawi ya miti punde magari yanapokuwa yameharibika. Kibaya ni kwamba wanapotengeneza magari yao huyaacha mawe au magogo katikati ya barabara na kuondoka zao. Hali hii imekuwa ikisababisha ajali na imekuwa chanzo kikuu cha uharibifu wa barabara.
Nukuu, "tuwe wastaarabu na wazalendo katika matumizi ya barabara, kuna madereva wanaweka Mawe na Magogo makubwa barabarani wanapoharibikiwa na magari, wakishatengeneza wanaondoka bila kuondoa mawe hayo au magogo hayo, huu sio uungwana, tabia hii inaharibu barabara zetu zilizojengwa kwa gharama kubwa na ni chanzo cha ajali"
Fikiria eneo la mlimani au kwenye kona kali, watu wanaweka Mawe makubwa yanawasaidia kutengeneza, wakimaliza hawayaondoi barabarani na kuondoka wanaacha palepale, huu sio ustaarabu, ni sawa na mtu aliyejisaidia naakacha choo bila kuflash, un civilization ya hali ya juu"
naagiza kwa nchi nzima Askari chukuen kumbukumbu kila magari yanapoharibika, wakiondoka bila kuondoa mawe wasilianeni popote watakapokuwa wamefika wakamatwe na wafike kwenye mkono wa sheria kwa kutengeneza mazingira ya ajali na kuharibu barabara" lazima tuwe na uzalendo na ustaarabu kwenze utunzaji wa barabara zetu na kujali usalama wa Raia wetu.
No comments:
Post a Comment