KIFO CHA AKWILINA NI MTAJI WA SIASA KWA
WANASIASA UCHWALA WA TANZANIA.
Na Peter Dafi.
Nazidi kusikitishwa na Kuumizwa kwa Kauli na Matendo ya wana
Siasa Uchwala wa Tanzania.
Tangu Binti Mrembo na mpole mwenye kila aina ya Sifa
alizokuwa nazo enzi za uhai wake, Kabla ya Kupoteza Uhai wake Kwenye Ghasia za
Tamaa za madaraka za Wanasiasa waliofanya Maandamano yasio na kibali huko
Kinondoni. Bado wana siasa hao hawajaridhika wanaendelea kusema na kufanya
Msiba wa Akwilina kama Mtaji wa Siasa zao za Maji Taka hapa Nchini Tanzania.
Haijawa mara ya Kwanza kwa CHADEMA Kufanya maandamano bila
Kibali wala Taarifa makusudi na kila wafanyapo hivyo basi Kifo au Vifo hutokea
bila kusahau Majeruhi, wizi ama uharibifu wa mali za Raia hutokea na baada ya
hapo! Hoja ya Msingi huwa ni Picha za Kifo na Majeruhi kupigwa nakuanza
kusambazwa kama mtaji kwao na kwa maboss wao wa Nje na Ndani ya Nchi.
Ndugu yangu kadili unavyoendelea Kusoma Ujumbe huu naomba
nikuulize!
Kwani kama CHADEMA wasingefanya maandamano Kifo cha AKWILINA
KINGEKUWEPO LEO HII?
Kama kweli CHADEMA ni waadilifu na wapenda Taratibu, Sheria,
Kanuni na Haki kwanini hawakutaka kufuata taratibu za Madai yao kwa Kuongozwa
na HEKIMA na BUSARA kwa Kufuata taratibu za maandamano ama Barua za kiofisi
kudai hizo haki zao? Ama kutuma watu wachache kufuatilia hizo Hati za Viapo?
Sasa Tizama Akwilina hakuwa kati ya Waandamanaji bali
alikuwa Mpita Njia tu akienda kupambana kutafuta ama kuijenga Future yake. Kaja
mwana kaifyatua na ikamtoa Uhai Binti na Kukatisha Ndoto zake zote na za FAMILIA
YAKE NA TAIFA KWA UJUMLA kwa KUPOTEZA NGUVU KAZI YA TAIFA.
Leo AKWILINA KAWA MTAJI WA SIASA hasa apale unapoona
wanasiasa Kila siku wanakuja na hoja za Waziri wa Ulinzi, Kamanda wa Kanda
Maalumu, Mkurugenzi nk… Wajiuzuru Kisiasa kwa kosa la Wachache kuamua kufanya
Maandamano tena wakijua wakifanya hivyo Mauwaji na majeruhi lazima watakuwapo,
Na kuthibitisha hilo Rejea Kauli za Mikutanoni, Kauli za Vingozi walipokuwa
tume ya uchaguzi siku mbili kabla ya uchaguzi wametamka sana Mauwaji Kutokea
Nk… Utaona kifo cha AKWIlINA kimekuwa sio Msiba tena bali ni mtaji wa Wanasiasa
na Hujipanga kufanya hivyo ili Kutafuta HURUMA ZA DAMU ZA WATU AMBAO HUPOTEZA
UHAI KWA GHASIA AMBAZO HUSABABIUSHWA NA HAWA WENZETU WA CHADEMA, iFIKE mahala
Watanzania Tujue Mbinu hizi na Tukemee kwa Pamoja.
Ningefurahi sana kama Tusingekuwa na HOJA YA KUWAJIBISHANA
KISIASA BADALA YAKE TUSHIRIKIANE KUMTAFUTA ALOFANYA TUKIO HILO HASAA…! IWE NI ASKARI AMA RAIA ALOKUWA NA BUNDUKI AMA
KIONGOZI MIONGONI MWA WALOKUWA WAKIANDAMANA ili Huyo kwanza apate Stahiki yake
yakufanya kosa la mauwaji kwa Makusudi ama kwa Bila kukusudia. Na iwe Fundisho
kwa Wakati Mwingine.
Manake Tusikimbilie Kuwajibishana kisiasa nakuacha Mzizi
wenyewe!
Tukumbuke Risasi Ilipigwa na mtu kwa Utashi wake akijua
anaenda kujeruhi ama kuuwa, Basi apatikane na tujue alitumwa na nani, Sio kukaa
nakuwasingizia Viongozi wa Jeshi la Police na CCM.
Lakini pia Tusisahau kuwa Kuna uwezekano kuwa Risasi ile
Ilikuwa ni Bahati mbaya kwa alokuwa na
Bunduki husika kumfyatuka ama kufyatua akiwa hana matarajio itaenda kupiga
kwenye Gari nakusababisha Kifo cha Binti AKWILINA.
Na hata kama ni Askari naomba ifahamike kuwa Kuvaa kwake unifomu
ya Jeshi la POLICE Haimfanyi kosa lake kuwa kosa la Askari ni kosa lake tu yeye
mwenye Mtu Binafsi na Hata maakamani atapanda mwenyewe na mashitaka atayajibu
yeye na sio Jeshi la police, na itakuwa hivyo kama ni Raia ndio kafanya hivyo
pia.
Wewe Unaesema kuwa huu ni mpango wa CCM na Police, Jiulize
Mtoto AKWILINA ameikoasea Nini CCM au Jeshi la Police Mpaka iamuriwe auwawe? Na
Tangu lini CCM na Police wakawa Wajamaa nakushirikianankufanya mauwaji? Think
Twice tusichume dhambi za Buree…!
Watanzanzia Tumekuwa tunajipa majibu na Hukumu ambazo
hatupaswi kujipa kabla ya kujua kweli, na Hatuwezi kwenda mbele kwa amani kama
tunataka kuishi kwa hisia.
WANASIASA ni watu Wabaya sana Wanaweza Lijenga ama kulibomoa
Taifa kwa Tamaa zao na subira zao, Kila
Chama ambacho kiko Nje ya madaraka Huhitaji kuingia madarakani kwa Namna yoyote
ile, iwe kwa UONGO, WIZI WA KURA, UHASI, MAPINDUZI Nk…. Ivyo Wanasiasa wako tayari kwa lolote ili wao wapate nafasi
serikalini au uongozi serikali, wenyewe husema Kumiliki Dola
Utaona Kauli za CDM zakupoteza uhai wa watu kwenye
maandamano na mikutano kwao sio issue sana ila issue ni ushindi wao tu! Ama kutimiza jambo husika.
Kinachofanyika na hawa wana CDM ni Kujenga Chuki kwa Raia
ili walichukie Jeshi la POLICE , Wawachukie watanzania wenzao ambao wanaamini
kwa CCM,
Baada ya Kifo cha Binti Akwilina utaona kaulI nyingi sana za
kichochezi zinaendelea kwenye Midomo ya Wanasiasa hawa, Kauli hizi zinakuwa ni
marudio ya kauli zao za awali ambazo walizisema mapema kabisa walipokuwa katika
kampeni kuwa Watu watakufa na kujeruhiwa, hii inatupa majibu na hisia kuwa
wamejipanga na walijipanga kufanya ama kusababisha haya kwa faida zao za
kisiasa.
Je! UNAJUA KUWA KUNA ASKARI WALIPIGWA MAPEMA KABISA KBLA
YAKUANZA KUWATAWANYA NA ASKARI HAO WAMELAZWA KWA MAJERAHA NA MAUMIVU MAKALI YA
KICHAPO CHA WAANDAMANAJI CHINI YA USIMAMIZI WA VIONGOZI WAO?
MWISHO. Niwaombe wanasiasa wa Tanzania kuwa waungwana walau
kwa baadhi ya mambo, Najua Tamaa za Uwongozi zinawasumbua sana lakini kumbukeni
Nafsi za wanaopoteza uhai zinasononeka sana, na Kusema uwongo ama kusingizia
Jeshi la Porisi ama kurushiana mipira kuwa ni CDM ama ni CCM haitasaidia sana
mwisho wa siku sisi wote ni mavumbi na Mavumbini tutarudi na Siku nya hukumu
itafika na kila mmoja atapata stahiki yake.
Tamaa za Uwongozi zisituondolee utu wetu.
Kifo cha Akwilina kisifanywe Mtaji wa Siasa, Msibani kuleta
Unafiki ni dhambi kubwa sana.
NB:- "Haya ni Maoni yangu yasihusishwe na mtu wala taasisi yoyote!"
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU AKWILINA MAHALA PEMA PEPONI! AMINA…….!!
Peter L. Dafi
MTETEZI WA WANYONGE
No comments:
Post a Comment