*MAVUNDE APOKEA MIFUKO 724 YA SARUJI KUTOKA CRDB BANK KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE KATIKA JIMBO LA DODOMA MJINI*
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh Anthony Mavunde* leo amepokea mifuko ya Saruji 724 yenye thamani ya *Tsh 10,000,000* kutoka *Benki ya CRDB* kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa,Nyumba za Walimu na matundu ya vyoo katika shule za Msingi na Sekondari katika Jimbo la Dodoma Mjini.
Akikabidhi mifuko hiyo ya Saruji,Mkurugenzi CRDB Tawi la Dodoma *Bi Rehema Hamis* amesema kwamba Benki ya CRDB inaunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano chini ya *Mh Rais Dr John Pombe Magufuli* na uchapakazi wa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde katika kuboresha miundombinu ya Elimu.
Akipokea mifuko hiyo ya saruji,Mbunge Mavunde ameishukuru benki ya CRDB kwa msaada huo ambao utalenga kupunguza changamoto ya ukosefu wa vyumba vya madarasa 1035 katika Jimbo la Dodoma Mjini ambapo kwa hivi sasa anaendesha kampeni maalum ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi na kwa kuanzia mfuko wa Jimbo umetoa matofali 32,000 na mifuko ya Saruji 2,560 kwa kata mbalimbali.
No comments:
Post a Comment