Bei ya bidhaa yazidi kupaa | Send to a friend |
Thursday, 23 February 2012 20:27 |
0diggsdigg Keneth GoliamaOFISI ya takwimu nchini imesema bei ya vyakula vingi imepanda kwa asilimia 26.2 ukilinganisha na mwaka jana ambapo ilikuwa ni asilimia 25.6 kipindi kama hiki.Taarifa hiyo inatolewa wakati wakazi wa miji mbalimbali wakiwamo wa Mbeya, Dar es Salaam , Dodoma, Mtwara na Mwanza wakilalamika juu ya kupanda kwa gharama za maisha hususan masuala ya vyakula. Ripoti kutoka Ofisi ya Takwimu iliyotolewa Februari 15 na kupatikana jana, bei ya vyakula nchini inazidi kupanda na kutishia maisha ya wakazi wake. Mkurugenzi wa Idara ya Takwimu ,Dk Albina Chuwa alisema hali ya kupanda kwa gharama ya vyakula bado ni kubwa.Licha ya ripoti kuonyesha bei ya vyakula kuendelea kupanda kwa kiasi kidogo, lakini hali ya gharama ya vyakula katika masoko jijini Dar es Salaam na Mbeya inazidi kupanda. “Matumaini ya kushuka kwa bei ya vyakula yanazidi kuota mbawa kutokana na hali ya bei inayozidi kupaa kila siku,’’ alisema. Nao wafanyabiashara wa maeneo mbalimbali jijini hapa walilalamikia kupanda kwa maisha pamoja na bei ya vyakula.Wafanyabiashara katika Soko la Buguruni walisema hatua ya kupanda bei ya vyakula kama nyanya, maharage mchicha, mchele na unga kunatokana na usimamizi mbaya wa uchumi nchini. Bei ya nyanya moja sasa ni Sh250, bei ya kilo moja ya maharage ni Sh 2,000, bei ya Sukari Sh2,500 kwa kilo na vishina vitatu vya mchicha ni Sh300, embe moja Sh800 wakati bei ya mananasi ni Sh2,000. Wakitoa maoni yao juu ya sababu za kupanda kwa bei hiyo walisema ni kutokana na kuongezeka kwa nauli ya usafirishaji wa mazao.Matha Mereni mfanyabiashara wa nyanya alisema jambo lingine linalochangia ni kuwapo kwa soko huria ambapo mazao mbalimbali sasa yamepata soko katika nchi za Afrika Mashariki. Naye Hamisi kajuru alisema Serikali imeshindwa kuzuia bei ya usafirishaji ndio maana Watanzania hasa wanaoishi jijini Dar es Salaam wanaendelea kupata maumivu ya bei ya vyakula kila siku. Lakini wengine walifafanua kwamba kuongezeka kwa bei ya vyakula kunatokana na kuongezeka kwa walaji wakati wazalishaji wakipungua.Walitoa wito kwa Serikali kutoa motisha kwa wakulima ili vijana wengi wakipende kilimo . |
No comments:
Post a Comment