Pages

Thursday, February 23, 2012

Machinga Wamtaka JK avunje bodi Machinga Complex

Wamtaka JK avunje bodi Machinga Complex  Send to a friend
Wednesday, 22 February 2012 20:46
Rais Jakaya Mrisho Kikwete

WAFANYABIASHARA wa Soko la Machinga Complex jijini Dar es Salaam, wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kuivunja  bodi ya soko hilo kwa madai kuwa imeshindwa kusimamia soko hilo baadhi ya wajumbe wake wakiendekeza rushwa.

Wakizungumza na maandishi wa habari hizi jana wafanyabiashara hao walidai kuwa uongozi wa soko hilo umeshindwa kuwahamisha wafanyabiashara wa Soko la Ilala  Mchikichini kutokana na baadhi yao kupewa fedha.

Walisema kuwa imefika wakati sasa kwa Rais Kikwekwe kuwaonea huruma kutokana na baadhi ya vigogo wa bodi hiyo kutumia soko la Ilala kujinufaisha  wakiliacha bila kulivunja  ili wenzao wahamie soko Machinga Complex kama wao.

“Umefika wakati kwa Serikali kuvunja Bodi ya Machinga Complex na kuteua bodi mpya itakayosaidia kufikia mwafaka. Haiwezekani  bodi  hiyo ishindwe kuwahamisha  wafanyabiashara  soko la Ilala kwa miaka miwili huku sisi tukiteseka Machinga Complex kwa kukosa wateja,” Steven Bukosi anayefanyabiashara katika soko hilo.

“Viongozi wakuu wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wanachukua pesa kwa wafanyabiashara wa soko la Ilala, ndio maana hata ukiongea mkuu wa mkoa ananyamaza kimya”alidai mfanyabiashara mwingine.

Walisema sababu kuu ya baadhi ya  wamachinga kushindwa kuingia Machinga Complex ni vigogo wengi kuchukua vizimba ambapo sasa inokekana kama vimejaa watu.

“Wanavunja kufuli na kuchukua kila kitu  halafu wanawapa watu ambao siyo wafanyabishara na hawafiki,” alisema Zuhura Wiliam kwa niaba ya wenzake.Alisema kuwa Jiji linaonekana kushindwa kuendesha soko hilo na kwamba ni bora wapewe na kuliendesha wao.


Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa  Soko  la Machinga Complex,  Abubakar Rakesh alisema viongozi wa juu wanajua mambo yote katika soko hili lakini wamekuwa  waoga.

Alisema  licha ya ushauri kutolewa kuhusu soko  hilo lakini hakuna kiongozi yoyote anayethubutu kufanyia kazi.
Alisema dhamira ya Rais Kikwete  kwa  wamachinga inanyanganywa  na wachache ambao hawataki kuona akina mama  wanaohangaika wananufaika na biashara zao ndogo ndogo.

Alisema lengo la kutaka kupangisha ghorofa ya nne na tano ya soko hilo ni kuruhusu wafanyabishara wachache kuwekeza na kuuza vitu vya jumla ili kuvutia wateja.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sadik Meck Sadiki   alipotafutwa kuzungumzia tuhuma hizo hakupatikana baada ya simu yake kuita bila majibu.

No comments:

Post a Comment