Pages

Thursday, September 27, 2012

Mgomo wa AngloGold Ashanti waenea Afrika Kusini



Mgomo uliokumba mojawapo ya migodi nchini Afrika Kusini wa dhahabu ,AngloGold Ashanti, sasa umeenea hadi katika migodi mingine ya kampuni hiyo nchini humo.
AngloGold imesema kuwa wengi wa wafanyakazi wake, takriban 35,000 nchini humo, wanashiriki katika migomo hiyo wakidai nyongeza ya mishahara.
Mgomo huu unajiri baada ya wafanyakazi wa kampuni ya madini ya Lonmin kurejea kazini wiki jana baada ya kugoma vile vile wakitaka mishahara mizuri.
Takriban watu 46 waliuawa wakati wa maandamano ya kudai nyongeza ya mishahara katika mgodi wa Marikana.
Uchunguzi wa mauaji hayo utaanza tarehe moja mwezi ujao.
Mgomo mwingine ambao hauhusiani na huu wa AngloGold, unaendelea katika mgodi mwingine wa dhahabu wa Gold Fields.
Mgomo huu wa AngloGold ulianza wiki jana katika mgodi wa Kopanang na kuenea hadi katika mgodi wa Mponeng ambao ndio wenye uketo mkubwa zaidi duniani.

No comments:

Post a Comment