Mgomo uliokumba mojawapo ya migodi nchini
Afrika Kusini wa dhahabu ,AngloGold Ashanti, sasa umeenea hadi katika
migodi mingine ya kampuni hiyo nchini humo.
AngloGold imesema kuwa wengi wa wafanyakazi
wake, takriban 35,000 nchini humo, wanashiriki katika migomo hiyo
wakidai nyongeza ya mishahara.Takriban watu 46 waliuawa wakati wa maandamano ya kudai nyongeza ya mishahara katika mgodi wa Marikana.
Uchunguzi wa mauaji hayo utaanza tarehe moja mwezi ujao.
Mgomo mwingine ambao hauhusiani na huu wa AngloGold, unaendelea katika mgodi mwingine wa dhahabu wa Gold Fields.
Mgomo huu wa AngloGold ulianza wiki jana katika mgodi wa Kopanang na kuenea hadi katika mgodi wa Mponeng ambao ndio wenye uketo mkubwa zaidi duniani.
Post a Comment